Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:33

Mahakama ya Kenya yawakuta na hatia Wairan wawili


Wairan wawili wakiwa mahakamani Kenya, Sayed Mansour Mousavi (kushoto) and Ahmed Abolfathi Mohammed, kulia
Wairan wawili wakiwa mahakamani Kenya, Sayed Mansour Mousavi (kushoto) and Ahmed Abolfathi Mohammed, kulia
Mahakama moja nchini Kenya imewakuta na hatia raia wawili wa Iran kwa kupanga kushambulia kiwa bomu vituo vya nchi za magharibi na Israel nchini Kenya.

Jaji Kaire Waweru alisema alhamis upande wa mashtaka umethibitisha bila ya mashaka tuhuma zote dhidi ya washtakiwa hao wawili.

Ahmad Abolfathi Mohammad na Sayed Mansour Mousavi walishtakiwa kwa kujiandaa kufanya uhalifu wenye nia ya uharibifu mkubwa baada ya kukamatwa Juni mwaka 2012 na kukutwa na maafisa wa usalama wakiwa na kilo 15 za milipuko aina ya RDX.

Mawakala hao wa Iran wanashutumiwa katika mashambulizi au kuandaa mashambulizi ulimwenguni kote katika miaka ya karibuni ikiwemo nchini Azerbaijan, Thailand na India. Njama nyingi ambazo zilibainisha kuilenga Israel.

Maafisa wa kupambana na ugaidi nchini Kenya walisema wa-Iran hao ni wanachama wa kitengo cha Islamic Revolutionary Fuards Corps Quds Force nchini Iran.
XS
SM
MD
LG