Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:29

Mahakama Kuu Marekani yaidhinisha sheria ya bima ya afya


Rais Barack Obama
Rais Barack Obama

Kwa kura ya 5-4 mahakama kuu imeidhinisha sheria hiyo ambayo italazimisha kila Mmarekani kuwa na bima ya afya ifikapo 2014

Mahakama Kuu ya Marekani imetoa uamuzi wa kihistoria Alhamisi kuhusu uhalali wa kisheria wa mswaada wa sheria ya bima ya afya - sera kubwa ya Rais Barack Obama.

Kwa kura 5-4 mahakama iliidhinisha sheria hiyo ambayo inataka wamarekani wote kuwa na bima ya afya ifikapo mwaka 2014 au watakabiliwa na adhabu ya faini. Jaji Mkuu John Roberts aliungana na majaji wenye sera za kadiri katika mahakama kuidhinisha sheria hiyo. Mahakama Kuu ambayo ina majaji tisa imegawanyika kati ya majaji watano wenye sera za kikonsevativu na wanne wenye sera za kadiri.

Sheria hiyo inalenga kutoa bima ya afya kwa zaidi ya Wamarekani millioni 30 ambao hadi sasa hawana bima, na ni ushindi mkubwa katika sera za ndani ya nchi kwa Rais Obama.

Mpinzani wa Obama katika uchaguzi ujao Mitt Romney wa chama cha Republican ambaye alipitisha sheria kama hiyo alipokuwa Gavana wa jimbo la Massachusetts, anapinga vikali sheria hiyo kitaifa. Romney ameahidi kubadili sheria hiyo akichaguliwa kuwa rais.

Wakizungumza katika baraza la Seneti la bunge la Marekani mara tu baada ya uamuzi wa mahakama viongozi wa chama cha Republican hawatatulia mpaka sheria hiyo inafutwa.

XS
SM
MD
LG