Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:54

Mafanikio ya Ziara ya Tillerson, Kelly Mexico


Waziri wa Usalama wa Ndani John Kelly akihutubia huko Mexico na kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson.
Waziri wa Usalama wa Ndani John Kelly akihutubia huko Mexico na kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson.

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson na Waziri wa Usalama wa Ndani John Kelly Mexico imeelezewa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kuboresha mahusiano na kupanga masuala ya mahusiano ya ujirani mwema kwa pande zote mbili.

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala ya ugaidi, usalama wa mipaka na biashara inayokadiriwa kufikia dola bilioni 1.5.

Pia ilikusudia kuainisha matakwa ya amri ya kiutendaji ya Rais Trump ya January 25 juu ya uhamiaji ambapo maelezo yalikuwa ni kuwaondoa kwa haraka wahamiaji wote walio haramu nchini Marekani.

Lakini maamuzi haya yanaathiri zaidi nchi ya Mexico hasa baada ya maelezo ya wizara ya mambo ya nje kwamba kama watu hawa hata kama sio raia wa Mexico, ili mradi wameingilia Mexico, watarudishwa nchini humo.

Mazungumzo ya Maelewano

Jambo ambalo limewaudhi sana maafisa wa Mexico na hivyo viongozi hao ikabidi waende kutuliza hali ya hewa nchini humo.

Kutokana na hali hiyo ilibidi wazungumzie hilo, kama ilivyo ripotiwa na vyanzo vya habari vya Marekani, na hasa kulainisha kauli na kuonyesha upole ambayo ndio nafasi ya diplomasia.

Hali ya mawaziri hao kutotumia ukali wa aina yoyote ile na kuonyesha mshikamano na maelewano kati ya serikali ya Marekani Mexcio ilikuwa ndio njia pekee ya kuwapooza viongozi wa nchi hiyo walionyesha kukasirishwa sana na amri ya kiutendaji.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili katika kipindi cha Kwa Undani ameeleza kuwa waziiri wa mambo ya ndani John Kelly ndipo alipo wahakikishia Mexico kwamba hakutakuwa na kurudishwa kwa mamilioni ya watu kama ilivyofikiriwa hapo awali.

Alisema kwamba Marekani imlenga kuondoa wahalifu tu na uondoaji watu utafanywa kwa uitaratibu na kuheshimu haki za binadamu.

Lakini wachambuzi wa mambo ya kidiplomasia wanasema ilikuwa ni muhimu sana kwa viongozi hao wawili kufanya haraka kuwafikia viongozi wa Mexico kwa sababu nchi hiyo sio adui wa Marekani bali ni mshirika wake wa kutegemewa.

Kiini cha Mazungumzo

Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la utafiti la Pew kunaakadiriwa raia wasio halali milioni 11.4 walihamia Marekani kutoka Mexico kwa mwaka 2014. Tatizo hili si geni isipokuwa Mexico imekuwa mshirika wa kusaidia Marekani katika kuzuia wahamiaji haramu waliopo Mexico. Kwa kweli jambo hili limemuathiri sana rais wa nchi hiyo Enrique Penya Nieto, kutokana na raia wake kumwona amekuwa mvumilivu sana kwa hayo mapendekezo ya Trump.

Lakini si hivyo tu Kwa mujibu wa Los Angeles Times, Mexico hivi sasa kuna raia wapatao milioni 1 wa Marekani wanaoishi nchini humo na hivi leo baadhi yao wametangaza kufanya maandamano kumpinga waziri wao wa mambo ya Nje Rex Tillerson.

Tillerson na Kelly kama nilivyoeleza hapo awali wamejaribu kuwahakikishia serikali ya Mexico kwamba hakutakuwa na uondoaji usiofuata haki za binadamu na kuongeza kwamba Marekani na Mexico ni washirika.

Lakini pia ni nchi mbili zilizo huru kwa hiyo hawawezi kukosa kutofautiana na kuongeza kwamba tumesikilizana kwa makini wakati tukizungumza masuala yetu kwa umakini mkubwa.

Tillerson pia aliongeza kwamba hakuna serikali inayoweza kufanya maamuzi dhidi ya serikali nyingine "anafahamu hilo."

Na kwa upande wa Mexico wao wamesema hawatakubali pendekezo hilo la Marekani na waziri wa mambo ya ndani wa Mexico Miguel Angel Osorio hakumung’umunya maneno kwa mujibu wa AP akisisitiza kutokukubaliana na Marekani. Akiongeza kwamba tumewaeleza wamarekani wasi wasi wetu kutokana na ongezeko la kufurusha watu nchini humo.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Mexico Luis Videgaray aliongeza kusema kwamba wasiwasi wetu ni kuheshimiwa haki za raia wetu tunaona utawala wa Trump unatekeleza sera ambazo zinaweza kuumiza watu wetu.

Makubaliano kati ya Marekani na Mexico

Tillerson kwa upande wake amesema kwamba utawala wa sheria ni muhimu kwa pande zote mbili za mipaka yetu akiahidi kushirikiana na Mexico katika kuzuia usafirishaji na uingizaji silaha haramu kwa pande zote za mpaka.

Mwandishi amesema kwa hiyo ukiliangalia kwa makini suala hili utaona kwamba kwa mujibu wa waziri wa Marekani ni wazi wana tofauti zao lakini anaona kwamba wataendelea kudumisha ushirikiano wao na Mexico na kushirikiana katika masuala ambayo hawana tofauti.

Pande zote zinakubaliana kwamba siuala la kuzuia uhalifu wa silaha na hasa madawa ya kulevya kati ya nchi zao mbili ni la msingi.

Imetayarishwa na Mwandishi Wetu Sunday Shomari, Washington, DC

XS
SM
MD
LG