Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:07

Bajeti ya Tanzania kujikita maeneo saba


Waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango
Waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango

Serikali ya Tanzania imesema katika bajeti ya mwaka huu 2017/18 inatarajia kuwa na ukomo wa Sh trilioni 31.6.

Kati ya fedha hizo za maendeleo kunaongezeko kutoka Sh trilioni 11.8 katika mwaka 2016/2017 hadi Sh trilioni 11.9 katika mwaka huu wa bajeti 2017/2018, ambalo ni sawa na asilimia 38 katika bajeti hiyo tarajiwa itakayosomwa Alhamisi wiki hii.

Mapendekezo ya bajeti ya 2017/18 yameainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miradi ya maendeleo inayolenga kufanikisha utekelezaji wa Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

Miradi ya maendeleo ni pamoja na ule wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga, ujenzi wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam, Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa kilomita 1,251 kwa kiwango cha standard gauge.

Pia ujenzi huo ni pamoja na matawi ya Tabora kupitia Isaka hadi Mwanza (kilometa 379), Isaka hadi Rusumo (kilometa 371), Kaliua kupitia Mpanda hadi Karema (Kilometa 321), Uvinza toka Hoima, Uganda hadi Tanga,Tanzania na kusomesha vijana wengi zaidi katika stadi za mafuta na gesi pamoja na uhandisi na uboreshaji huduma za afya.

Kwa mujibu wa Wiziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango maeneo mengine ni viwanda vya kukuza uchumi wa viwanda, kuwianisha maendeleo ya uchumi na ya watu na mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji.

Eneo lingine muhimu ni uendelezaji sekta za ubia kati ya sekta ya umma na binafsi pamoja na maeneo mengine muhimu kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa.

Wizara pia imesma lengo la uandaaji wa mpango wa bajeti, unaongoza serikali katika kusimamia mambo ya uchumi ikiwamo kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa kufikia asilimia 7.5 katika mwaka huu, asilimia 7.9 mwakani na asilimia 8.2 mwaka 2019.

Aidha mpango huo unalenga kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kubaki na tarakimu moja hadi kufikia asilimia 5.0 katika kipindi cha muda wa kati, kuwa na pato ghafi la taifa la Sh trilioni 123.9 kwa mwaka 2017/18, Sh trilioni 139.7 kwa mwaka 2018/19 na Sh trilioni 165.4 mwaka 2019/20. Pia mapato ya kodi kufikia asilimia 14.6 ya pato la taifa mwaka 2017/18, asilimia 15.5 mwaka 2018/19 na asilimia 15.8 mwaka 2019/20.

XS
SM
MD
LG