Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:59

Maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi yafanyika Marekani


Maandamano Washington Dc Alhamisi Julai 7,2016.
Maandamano Washington Dc Alhamisi Julai 7,2016.

Na Sunday Shomari na Mary Mgawe.

Maelfu ya wakazi wa jiji la Washington DC wameandamana walipokutana kwenye bunge la nchi hiyo - Capitol Hill, wakitoa wito kwa wabunge kuungana nao kupinga vifo vya wamarekani weusi wawili waliouwawa na polisi wiki hii.

Watu hao walikusanyika wakiwa wamefuatana na wabunge wa Marekani wakiimba na kubeba mabango kupinga mauaji dhidi ya watu weusi.

Watu wa aina mbali mbali walijitokeza weusi kwa weupe kuandamana kwa nia moja ya kupinga mauaji hayo na kudai haki itendeke.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:33 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Video zilizopigwa kwa njia ya simu zilimwonyesha Alton Sterling mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Baton rouge Luoisiana akiangushwa na Polisi na kupigwa risasi.

Na mtu mwingine Philando Castile wa St. Paul Minnesota mwenye umri wa miaka 32 alipigwa risasi mbele ya mchumba wake na mtoto baada ya kusimamishwa na Polisi kutokana na kosa la kukaribika taa kwenye gari lake kwa mujibu wa CNN.

Baada ya kupigwa risasi mchumba wa marehemu alianza kurekodi kwenye face book moja kwa moja kwa njia ya simu yake.

Marehemu alionekana kwenye gari akitokwa na damu nyingi na huku polisi akiwa amemshikia bunduki kwenye upande wa dirisha lake.

Wakati huo huo kwa mujibu wa CNN inaripotiwa Polisi watatu wamefariki dunia na wengine kumi na moja kujeruhiwa katika maanadamano ya kupinga mauaji hayo jijini Dallas Texas.

Inaelezwa kuwa watu wawili wenye silaha walijitokeza na kushambulia polisi hao , watu hao bado hawajulikani walipo na Polisi wanaendelea kuwatafuta wakiripotiwa kuzunguka eneo hilo kujaribu kumkamata mmoja wa washambulaiji hao.

XS
SM
MD
LG