Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:48

Maafa nchini Norway


Maafisa wa uokoaji wakimsadia muathiriwa wa mashambulizi katika ksiwa cha Utoeya, Norway.
Maafisa wa uokoaji wakimsadia muathiriwa wa mashambulizi katika ksiwa cha Utoeya, Norway.

Watu 91 wauawa katika mashambulizi nchini Norway

Polisi wa Norway wanaendelea na uchunguzi kubaini ikiwa kuna mtu wa tatu mwenye bunduki aliyehusika katika mashambulizi ya Ijumaa katika kambi ya vijana ambapo watu 91waliuawa. Polisi wanaendelea kumhoji mtu mmoja aliyekuwa na bunduki raia wa Norway, lakini shirika rasmi la habari nchini humo NTB limesema Jumamosi kuwa walioshuhudia shambulizi hilo katika kisiwa cha Utoeya wamewaambia polisi kulikuwa na washambuliaji wawili. Mmoja ambaye amekamatwa na kuzuiliwa na polisi alikuwa amevalia sare kama za polisi lakini wa pili alikuwa amevaa mavazi ya kiraia. Norway imo katika hali ya mshtuko mkubwa kutokana na mashambulizi mawili ya Ijumaa yaliyosababisha vifo vya watu hao 91, 7 miongoni mwao katika mlipuko mkubwa wa bomu kwenye makao makuu ya serikali mjini Oslo na 84 wakiuawa kwa kupigwa risasi katika kambi ambapo vijana walikuwa wamekusanyika kwa program iliyodhaminiwa na chama tawala cha Leba. Waziri Mkuu Jens Stoltenberg alisema ni mashambulizi yenye maafa makubwa kuwahi kutokea Norway tangu vita vya pili vya dunia na kuyaita mkasa wa kitaifa usioeleweka. Alishtumu mashambulizi hayo ya bomu na risasi akisema ni ya umwagaji damu katika kisiwa cha furaha kilichogeuzwa kuwa cha majonzi.

XS
SM
MD
LG