Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:41

"Live Talk" Siasa za Mombasa na mustakbal wake


Wafuasi wa Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho wakisherekea ushindi wake Marchi 2013
Wafuasi wa Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho wakisherekea ushindi wake Marchi 2013
Chini ya mfumo mpya wa utawala wa madaraka nchini Kenya, County mpya zilizoundwa kutokana na katiba mpya, zinaripotiwa kukabiliwa na matatizo ya matumizi mabaya ya fedha, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na mivutano ya kisiasa.

Mombasa ni moja wapo za County muhimu za Kenya inayokumbwa na mvutano mkubwa wa kisiasa wakati utawala wa Gavana Ali Hassan Joho unakosolewa kwa kumaliza sehemu kubwa ya fedha kutoka serikali kuu kabla ya muda uliowekwa.
please wait

No media source currently available

0:00 0:46:40 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mbali na matatizo ya uwongozi wtumishi wa serikali ya County hawajalipwa mishahara yao kwa miezi miwili sasa, na kuongeza mafuta kwenye moto, Gavana Joho anatokea kutoka Muungano wa kisiasa CORD ambao ni wapinzani wa serikali kuu ya Mungano wa Jubilee na hivyo kusemekana kuna kutoelewana hapo na serikali kuu ya Nairobi.

Joho tayari ameshfanya mabadiliko katika baraza lake la utawala na kuutaka upinzani kumpa nafasi ya kutekeleza majukumu ya wananchiwa Mopmbasa. Lakini Upinzani umemfikisha mahakamani kwa magai kwamba amewasilisha cheti kisicho cha kweli cha masomo yake ya juu na wanataka aondolewe madarakani.

Basi katika Live Talk Bw .Ali Bafundi Ali diwani wa zamani wa Bondeni Salim Bajaber diwani wa zamani wa Tudor na Zubeir Noor mchambuzi wa masuala ya kisiasa, wanazungumzia mivutano hiyo ya kisiasa za Mombasa na athari zake kwa siasa jumla za Kenya.
XS
SM
MD
LG