Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:01

Profesa Lipumba asema katiba ya CUF inamruhusu kurejea kwenye uongozi


Profesa Ibrahim Lipumba kiongozi wa chama cha upinzani CUF Tanzania.
Profesa Ibrahim Lipumba kiongozi wa chama cha upinzani CUF Tanzania.

Wanachama wa chama wa wananchi CUF mjini Dar es salaam, Tanzania wamedai kwamba chama chao kilipoteza mwelekeo wa kisiasa baada ya aliyekuwa mwenyekiti profesa Ibrahim Lipumba kujiweka kando mwaka jana kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo.

Ripoti ya Dina Chahali
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:51 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika makao makuu ya chama hicho Buguruni Jijini Dar es salaam shangwe na nderemo ziliibuka kwa wanachama na washabiki wa CUF baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho prof. Ibrahim Lipumba kutangaza kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu kama mwenyekiti wa chama hicho na kurejea kwenye uongozi.

Akizungumzia kurejea kwake kwenye uongozi Profesa Lipumba alisema katiba ya chama cha CUF inamruhusu kwa vile barua yake ya kujiuzulu aliyoandika kwa katibu mkuu na kwa baraza la uongozi la chama hazikujibiwa mpaka sasa anapochukua uamuzi huo na hivyo baada ya kuombwa na watu mbalimbali ameamua kurejea kwenye uongozi wake.

Akizungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa nchini humo Profesa Lipumba alionekana kuguswa na kile alichokiita matukio ya kuminya demokrasia yanayoendelea nchini hivi sasa.

Prof. Lipumba aliondoka kwenye uenyekiti CUF takribani miezi kumi iliyopita baada ya kuwepo msuguano kwenye Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) wakati wa kumpata mgombea mmoja wa kiti cha urais kupambana na mgombea wa chama cha mapinduzi- CCM.

XS
SM
MD
LG