Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:15

Libya yasherehekea siku ya Ukombozi


Wa-Libya wakiwakaribisha wapiganaji wa mapinduzi kutoka Misrata wakiwasili Benghazi, Oktoba 22, 2011.
Wa-Libya wakiwakaribisha wapiganaji wa mapinduzi kutoka Misrata wakiwasili Benghazi, Oktoba 22, 2011.

Viongozi wa Libya na wananchi wanasherehekea siku ya ukombozi mjini Benghazi kufuatia kuuliwa kwa kiongozi wa zamani Muammar Ghadafi na kufikisha kikomo utawala wake wa miaka 42

Ni siku nyingine ya kihistoria kwa Wa-Libya pale viongozi wa Baraza la Mpito la Kitaifa, NTC likiongozwa na mwenyekiti wake Mustafa Abdel Jalili walipotangaza Jumapili Oktoba 23 ni siku ya ukombozi wa Libya na siku ya mashujaa.

Maelfu na maelfu ya watu wamemiminika kwenye uwanja mkuu wa Benghazi mji wa mashariki ambako vuguvugu la mapinduzi lilinazia. Inaripotiwa wapiganaji kutoka miji mbali mbali wamewasili kuhudhuria sherehe hizo.

Viongozi wa NTC walitangaza siku ya ukombozi kufuatia kuuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gadhafi siku ya Alhamisi.

Wakati sherehe zikiendelea Jumuia ya Kimatiafa ingali inataka kufahamu jinsi kiongozi huyo alivyofariki. Madaktari walochunguza mwili wa kiongozi huyo mjini Misrata wanasema alifariki kutokana na majereha ya risasi.

XS
SM
MD
LG