Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:04

Viongozi wa Libya na Misri kukutana Khartoum


Wakazi wa Sudan kusini wakiwasili katika mji mkuu Juba wakitokea Khartoum kabla ya upigaji kura ya maoni ya Januari 9, juu ya uhuru wa Sudan kusini
Wakazi wa Sudan kusini wakiwasili katika mji mkuu Juba wakitokea Khartoum kabla ya upigaji kura ya maoni ya Januari 9, juu ya uhuru wa Sudan kusini

Viongozi kutoka Libya na Misri watatembelea Khartoum Jumanne kwa mazungumzo na Rais wa Sudan Omar al-Bashir juu ya hali ya baadaye nchini kwake.Mkutano huo unafanyika kabla ya kura ya maoni ya Januari 9 kuamua juu ya uhuru wa Sudan kusini ambao unaelekea kuligawa taifa hilo sehemu mbili.

Misri na Libya ambao ni jirani na Sudan wangependa kuzuia machafuko yeyote ya uhamiaji kama vita vitatokea ikiwa ni matokeo ya uhuru wa Sudan Kusini. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linabashiri kwamba zaidi ya watu milioni moja watakoseshwa makazi.

Jumapili Rais wa Marekani Barack Obama alituma barua kwa viongozi wa kieneo barani Afrika kuwasihi kuunga mkono kura ya maoni ifanyike kwa amani.


Mivutano kati ya waislam walio wengi upande wa kaskazini na wakristo wachache wa kusini imeongezeka kabla ya upigaji kura kuwadia na migogoro kuhusu kodi ya mafuta, mipaka na masuala mengine haijatatuliwa.

Jumapili Rais Bashir alisema nchi hiyo itaidhinisha katiba ya kiislam na kwamba kiarabu kitakuwa lugha rasmi kaskazini, endapo kusini itapiga kura ya kuwa taifa huru.

Kura ya maoni ni sehemu muhimu ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza miaka 21 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Sudan kaskazini na kusini.



XS
SM
MD
LG