Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:48

Kifo cha Younes chaleta mvutano Benghazi, Libya


Abdel Fattah Younes, mkuu wa jeshi la upinzani nchini Libya ameuwawa Alhamis na watu wasiojulikana nchini humo
Abdel Fattah Younes, mkuu wa jeshi la upinzani nchini Libya ameuwawa Alhamis na watu wasiojulikana nchini humo

Mji mkuu wa Benghazi ambao ni ngome ya waasi nchini Libya ulikumbwa na mvutano Ijumaa baada ya kuripotiwa mashambulizi ya risasi katika mitaa ya Benghazi kufuatia maandalizi ya mazishi ya mkuu wa jeshi la upinzani aliyeuwawa.

Baraza la uongozi la uasi linasema kamanda wake wa jeshi wa cheo cha juu Abdel Fattah Younes na wafanyakazi wake wawili waliuwawa na watu wasiojulikana Alhamis.

Mkuu wa baraza la kitaifa la mpito Mustafa Abdel Jalil alisema kwamba Younes na wafanyakazi wake hao wote makanali waliuwawa kabla ya kufika kuhojiwa kwenye kesi ya kamati ya upinzani ya sheria kuhusu suala la jeshi. Alisema mkuu wa gereza hilo ambaye aliwauwa watu hao alikamatwa.

Jalil hakuwa wazi kuelezea nani anayemuhisi alihusika na shambulizi hili. Anasema waasi watafanya siku tatu za maombolezi.

Waasi walisema walimkamata Younes kufuatia wasi wasi kuwa familia yake huwenda bado inaushirikiano na washirika wa karibu wa bwana Gadhafi.

Younes alikuwa waziri wa mambo ya ndani nchini Libya na mmoja wa washirika wa karibu wa upinzani kabla ya kubadilisha ghafla msimamo wake kuelekea upinzani mwanzoni mwa ghasia ambazo zilianza mwezi Februari.

XS
SM
MD
LG