Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:48

Marekani yaadhimisha siku ya mashujaa


Baadhi ya wanajeshi wa Marekani wakiwa katika vita nje ya nchi yao katika harakati za kuilinda nchi yao
Baadhi ya wanajeshi wa Marekani wakiwa katika vita nje ya nchi yao katika harakati za kuilinda nchi yao

Rais Obama atalitembelea eneo la Vietnam Veterans pamoja na makaburi ya kitaifa ya Arlington kutoa heshima kwa wanajeshi waliokufa wakati wa vita

Rais wa Marekani Barack Obama anapanga kuwatunukia heshima wanajeshi waliokufa wakati wakihudumu katika vita kwa kutumia sherehe za siku ya mashujaa kwa kuungana na familia zao huku jamii kote nchini zikifanya sherehe zao wenyewe.

Rais atatembelea eneo la kumbukumbu la Vietnam Veterans pamoja na makaburi ya kitaifa ya Arlington yaliopo nje kidogo ya Washington ambapo wanajeshi wameweka bendera za Marekani kwenye makaburi takribani 260,000.

Maadhimisho makubwa ya kwanza ambayo awali yaliitwa Decoration Day yalifanyika kwenye makaburi hayo mwaka 1868 miaka mitatu baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 600,000.

Bwana Obama alisema katika hotuba yake ya kila wiki kwamba sikukuu ni muda ambao nchi inawatunukia heshima wale ambao walijitoa mhanga na kuthibitisha nia yao ya dhati kuwahudumia wale ambao walirudi nyumbani.

Wamarekani wengi hawafanyi kazi na shule zimefungwa ambapo wikiendi ndefu inaonekana kama mwanzo usio rasmi wa kipindi cha mapumziko ya majira ya joto. Sherehe hizi zinajumuisha mkusanyiko wa watu katika bustani za mapumziko au safari za kuelekea ufukweni.

XS
SM
MD
LG