Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:11

La Nina huenda ikasababisha ukame Afrika Mashariki


Picha za satelite zilizotolewa na NASA April 21, 2008 zikionyesha moja La Nina zenye nguvu katika miaka kadhaa katika baghari ya Pacific karibu na equator.
Picha za satelite zilizotolewa na NASA April 21, 2008 zikionyesha moja La Nina zenye nguvu katika miaka kadhaa katika baghari ya Pacific karibu na equator.

Miaka mitano iliyopita athari za La Nina mfumo wa hali ya hewa katika eneo la Pacific ilifikia pembe ya Afrika na kusababisha ukame mkubwa. Mwaka huu wansayansi wa hali ya hewa wanasema inaonekana kama La Nina inarudi tena.Hiyo ni habari mbaya kwa eneo lililopigwa na ukame la magharibi mwa Marekani lakini pia inaweza kumaanisha ukame kwa maeneo yalio mbali kufikia maeneo ya Afrika mashariki, kati na kusini na pia mashariki mwa China.

Bahari ya Pacific iko kati kati ya hali ya hewa ya el nino ambayo inapelekea joto eneo la chini la bahari lakini wanasayansi wa hali ya hewa hawasemi zaidi.

Inatarajiwa kuchukua nafasi ya La Nina ambayo inatuliza sehemu ya chini ya bahari katika eneo la kati na mashariki mwa bahari ya Pacific inatokea kila baada ya miaka miwili hadi mitano.

Mwanasayansi mtafiti wa Jiolojia wa Marekani Dr.Chris Funk anasema pamoja na kuonekana ni jambo la ajabu mifumo yote ya hali ya hewa inaweza kuathiri mifumo ya muda mrefu ya hali ya hewa katika nchi isiyo na bahari kiasi cha umbali wa eneo la upande mwingine wa dunia.

Dr.Funk anasema "wanasayansi huko NOAA wanatabiri kwamba El Nino inaweza kuondoka mara moja na kuchukuliwa na El Nina na kiasi cha asilimia 75 ya nafasi inaweza kutokea kipindi cha Kipupwe . Kama ikitokea hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba tutakuwa na ukame kusini mwa Ethiopia ifikapo Kipupwe cha mwaka ujao".

Fikiria kama maandazi yaliopangwa moja likianguka , yote yanaanguka na wakati hali ya hewa ikibadilka huko ukanda wa Pacific mabadiliko hayo yanaporomoka dunia nzima.

Kwa sasa El Nino ni sehemu ya sababu kwamba sehemu ya kaskazini ya Ethiopia inakumbana na ukame mbaya kuliko kuwahi kutokea katika miongo kadhaa. Lakini wakati La Nina inachukua mkondo wake Funk anasema huo ukosefu wa mvua unaweza kuelekea katika maeneo ya kusini ya Ethiopia ambayo yanakwenda mpaka pembe ya Afrika.

Dr.Funk Unajua kuna misimu miwili tu ya mvua katika eneo la Equatorial la Afrika Mashariki. Wanapata mvua wakati wa Kipupwe , Oktoba , Novemba na Desemba na kuna msimu mwingine wa mvua mwezi machi, Aprili na Mei. Kwahiyo moja ya hatari za La Nina inaweza kufanya hii misimu yote kuwa mibaya.Hicho ndicho kilichotokea mwaka 2010 na 2011.Kuna wasi wasi kwenye mtazamo wa suala la usalama wa chakula kwa hiyo tunaweza kuwa misimu miwili dhaifu ya mvua".

Ukame wa mfululizo katika nchi za Kenya na Somalia au ukame wa Machi mpaka Juni huko Ethiopia, unaweza kusababisha ukosefu wa chakula na maji kuathiri vituo vya kuzalisha umeme na maji na kudhoofisha hali ya kilimo.

Timu ya Funk inafanya kazi juu ya njia za kujiandaa na hali ya ugumu. Wanawataka wananchi kujiandaa na kupoteza fedha kutokana na ukame lakini pia wanataka vifaa vya hali ya juu kusaidia wakulima na mameneja wa mifugo kutafuta maji.

Dr.Funk anasema " Swali lako la bima ya mifugo ni zuri sana na moja ya mambo tunayofanyia kazi ni uweza wa kutumia taarifa za satellite za hali ya juu ili kusaidia ufugaji kwenye ardhi ya rutba mradi huo unafanya kazi”.

Pengine hatutaweza kuzuia ukame lakini wanasayansi wanaendelea kuwa na uweza wa kutabiri ukame na kusaidia wale walioathirika zaidi kujiandaa kwa hali mbaya zaidi.

XS
SM
MD
LG