Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 00:26

Kundi la IS linadai kuhusika na shambulizi la Indonesia


Mgahawa wa Starbucks mahala ambako shambulizi hilo lilitokea nchini Indonesia
Mgahawa wa Starbucks mahala ambako shambulizi hilo lilitokea nchini Indonesia

Wanamgambo wa kundi la Islamic State wanadai kuhusika na shambulizi la Alhamis katika mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta shambulizi ambalo lilisababisha vifo vya watu saba wakiwemo washambuliaji watano.

Shirika la habari la Aamag lenye uhusiano na wanamgambo wa Islamic State-IS lilisema shambulizi katika mtaa wa matajiri wa Jakarta liliyalenga mataifa ya kigeni na vikosi vya usalama vinavyofanya kazi kuwalinda. Wageni walikuwa miongoni mwa watu 20 waliojeruhiwa.

Polisi wa Indonesia wakiimarisha usalama baada ya tukio, Jan. 14, 2016.
Polisi wa Indonesia wakiimarisha usalama baada ya tukio, Jan. 14, 2016.

Awali msemaji wa polisi wa Indonesia, Anton Charliyan alisema kundi lenye uhusiano na IS huwenda lilihusika na shambulizi hilo na washambuliaji walionekana kujaribu kufuata mashambulizi ya ugaidi yaliyofanyika mwezi Novemba mjini Paris nchini Ufaransa. Mkuu wa polisi wa Jakarta, Tito Karnavian alieleza kwa kina akimtaja raia mmoja wa Indonesia nchini Syria kuwa anahusika. Viongozi wote wa Islamic State huko kusini-mashariki mwa Asia wanashindana kuwa wakuu katika kanda hiyo.

Na Kulingana na ripoti za usalama, kundi la IS limekuwa likitoa mafunzo nchini Indonesia taifa lenye idadi kubwa sana ya waislam duniani. Mamia ya wa-Indonesia wameondoka nchini humo kujiunga na kundi nchini Syria.

Kwa mujibu wa Greg Fealy, professa kwenye chuo kikuu cha taifa cha Australia ambaye anasomea ugaidi nchini Indonesia, amesema kitisho cha ugaidi cha IS nchini Indonesia kimeongezeka tangu kati kati ya mwaka 2004.

XS
SM
MD
LG