Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:26

Huduma ya kifedha kwa simu yabadilisha uchumi wa Kenya


Mengi yamesemwa kuhusu teknologia ya kutuma fedha kutoka mtu mmoja hadi mwengine kupitia simu za mkononi, yani m-pesa na jinsi inavyobadilisha uchumi wa Kenya. Hivi sasa teknologia hiyo inasemekana inauwezo wa kuwasaidia wajasiri mali kuimarisha biashara zao kufikia kiwango cha juu .

Kulingana na mratibu wa kampuni ya teknologia ya Sage tawi la Afrika mashariki na magharibi Dkt Rutendo Hwindigwi, kupanuka kwa kasi mfumo wa kutuma pesa kupitia simu kote nchini Kenya na hivi sasa kuenea katika mataifa jirani kunasaidia kuimarisha ujasiri mali pamoja na kufanyika kwa ustadi zaidi biashara ndogo ndogo.

Dk Hwindingwi anasema faida moja kubwa ya teknologia hiyo imewezesha biashara ndogo ndogo na hata wachuzi na bishara za wastani zisizo na akauti za benki kufanya biashara zao kwa kutumia mfumo wa malipo kwa kutumia simu.

Amesema kuwa teknologia hiyo imepunguza muda unaotumika kulipana fedha miongoni mwa watu na pia kutoa usalama wa kibiashara huku masoko mapya yakijitokeza. Kwa mujibu wa halimashauri ya mawasiliano ya Kenya, nchi hiyo ni miongoni ya mataifa ya kwanza kutumia teknologia ya kutumia simu kutuma fedha na kwamba shilingi bilioni 3 hulipiwa kwa njia ya kutumia simu kila siku. Kenya inashikilia asilimia 58 ya teknologia hiyo barani Afrika. Licha ya kiwango hicho, bado kuna nafasi kubwa ya ukuaji huko Kenya.

Dkt Hwindigwi anasema kulingana na utafiti uliofanywa na kampuni ya Nielsen, asilimia 95 ya wakenya wangali wanatumia fedha taslimu, asilimia 12 wanatumia simu kufanyia malipo huku asilimia 2 pekee wakitumia kadi za benki.

Anasema biashara ndogo ndogo na za wastani hasa katika bishara zamaduka na usafiri kutaweza kuimarisha utumiaji wa fedha kupitia simu za mkononi.

Amesema kwa kutumia pesa taslimu kuna madhara yake. Teknologia ya kulipia ya kidigitali ni salama na haihitaji mtu kuweko binafsi ili kuweza kulipa. Wizi wa pesa taslimu pia unapunguzwa na teknologia hiyo. Ameongeza kusema kuwa teknologia ya kutumia simu za mkononi kufanya malipo sasa haifanyiki kati ya watu binafsi tu bali hata makampuni yameanza kufanya biashara kwa kutumia teknologia hiyo. Dkt Hwindigwi anasema mustakbal wa biashara ni simu za mkononi na hivyo kampuni yake inawapa uwezo wateja wake kufanya biashara zao kwa kutumia simu na kwa hivyo kurahisisha mambo na kufanya mazingira ya kibiashara kuwa salama.

XS
SM
MD
LG