Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 06:35

Korea Kusini yahofia kushambuliwa na ISIS

Korea Kusini inachukua hatua za kuongeza usalama ili kuzuia uwezekano wa shambulizi kutoka Islamic State (IS) baada ya Idara ya Ujasusi ya nchi hiyo kuonya kwamba kundi hilo la kigaidi huwenda linalenga vituo vya kijeshi vya Marekani pamoja na raia kwenye peninsula ya Korea.

Idara ya Ujasusi ya taifa ya Korea Kusini (NIS) ilisema jana Jumapili kwamba IS ilitoa orodha ya malengo muhimu ya kushambuliwa ambayo yanajumuisha vituo vya kikosi cha anga namba 77 cha Marekani na NATO katika nchi 21 na pia watu muhimu wanaohisiana nao.

Vituo vinne vya jeshi vilivyopo kwenye orodha ya malengo ya IS yapo Korea Kusini.

NIS iliripoti kwamba orodha ilikua na habari kamili za mahala vituo vinapatikana na picha za satelaiti kutoka ramani ya Google ya kambi ya jeshi la anga la Marekani huko Osan, jimbo la Gyeonggi na mji wa Gunsan huko Jeolla Kaskazini.

XS
SM
MD
LG