Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:38

Korea Kaskazini yafanya tena uchokozi wa makombora


kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un
kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un

Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wamesema, Korea Kaskazini Jumatano ilirusha makombora mawili kutoka pwani ya mashariki ambapo moja kati ya majaribio hayo mawili lilishindikana.

Makombora hayo mawili yalirushwa mapema Jumatano na inaaminika kuwa ni kombora la masafa ya kati linalojulikana kama Musudan ambalo lina uwezo wa kufikia kambi za kijeshi za Marekani huko Asia na Pacific.

Korea Kaskazini ilifanya jaribio bila mafanikio la kurusha makombora kama hayo mara tatu mwezi Aprili. Jaribio jingine ambalo linadhaniwa kuwa ni Musudan halikufanikiwa mwezi Mei.

Wakati huo huo Jeshi la Japan lilikuwa kwenye tahadhari ya makombora hayo na makombora yake ya jeshi ya Patriot yaliamriwa kuangusha kombora lolote lile kuelekea Japan kwa mujibu wa chanzo cha habari cha serikali.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilipiga marufuku Korea kaskazini kutengeneza silaha za nyumklia na makombora ya masafa marefu .

China ambayo ni mshirika mkubwa wa Korea kaskazini ilitoa wito kwa Rais Kim Jong Un kurejea katika maelekezo ya mazungumzo ya kimataifa na kuacha programu zake za nyuklia kwa ajili ya msaada wa kiuchumi na uhakika wa usalama.

XS
SM
MD
LG