Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:32

Marekani juu kwenye kombe la dunia.


Nahodha wa timu ya wanawake ya Marekani Carli Lloyd akisherehekea goli kwenye mchuano dhidi ya Japan.
Nahodha wa timu ya wanawake ya Marekani Carli Lloyd akisherehekea goli kwenye mchuano dhidi ya Japan.

Nahodha wa timu ya marekani, Carli Lloyd alijipatia mabao matatu ikiwemo lile ambalo alilifunga kutoka mbali, na hivyo kuifanya marekani kuongoza kwa mabao manne kwa bila katika michuano ya wanawake ya kombe la dunia na kumshinda kwa urahisi bingwa mtetezi Japan mabao 5–2 mjini Vancouver, Canada.

Hakuna timu yoyote iliyowahi kufunga zaidi ya magoli mawili katika fainali za kombe hilo, lakini Lloyd alifanya hivyo katika muda wa dakika 16 za mchezo. Bao la ufunguzi lilipatikana katika dakika ya tatu wakati Megan Rapinoe aliposukuma pasi safi na Lloyd akiwa ameitaimu vyema na kupiga mkwaju mkali, ambao ulimpita mlinda lango wa Japan, Ayumi Kaihori.

Japan ilishangaa pale dakika mbili baadaye Lloyd alipotia bao lingine kinywani.

Mpira mwingine wa chini kwa chini ulioharibu mambo kwa Japan, safari hii ulitoka kwa Lauren Holiday ambaye alipiga free kick ambayo walinzi wa Japan walishindwa kuipangua. Mpira ulimfikia Lloyd na kuusukuma kwenye goli la wapinzani.

Timu ya Japan haikuwa na muda wa kujiweka sawa kabla ya kujikuta wakipigwa bao lingine la tatu katika dakika ya 14, pale mchezaji wa Japan Azusa Iwashimizu alipoupiga mpira na kumfikia Holiday na kuuvurumisha golini. Marekani iliongoza kwa mabao 4 – 2.

Lakini katika dakika ya 52 Japan iliweza kujipatia bao la pili pale mpira wa kichwa uliopigwa na Julie Johnston ulimpita mlinda lango Hope Solo na kwenda moja kwa moja kwenye nyavu ya marekani. Lakini muda mfupi baadaye marekani ilipata bao la tano. Ushindi huu wa marekani unaondoa kumbu kumbu za kuchapwa kichapo na Japan katika fainali za mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG