Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:05

Kiongozi wa waasi Riek Machar ameapishwa mjini Juba


Rais Salva Kiir (L) akipeana mikono na Makamu Rais wa kwanza Riek Machar.
Rais Salva Kiir (L) akipeana mikono na Makamu Rais wa kwanza Riek Machar.

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar alirejea katika mji mkuu wa Juba siku ya Jumanne na kula kiapo kama Makamu Rais wa kwanza.

Kuwasili kwa Machar kumeongeza matumaini kwamba serikali na waasi wanaweza kusonga mbele na mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka jana wa kumaliza miezi 30 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Baada ya kuapishwa, Rais Salva Kiir alisema yeye na Machar haraka wataendelea kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, kulingana na mkataba wa Amani. Alisema hili ni chaguo pekee la kurudisha Sudan Kusini kwenye njia ya umoja na mafanikio.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:46 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakati huo huo bwana Machar katika matamshi yake, aliahidi kushirikiana na Rais Kiir. Bwana Machar aliwahi kuwa Makamu Rais wa Kiir na alifutwa kazi Julai mwaka 2013 jambo ambalo lilizusha vita mwezi Disemba mwaka huo huo.

Tangu wakati huo mapigano yameuwa maelfu ya raia wa Sudan Kusini na kuwakosesha makazi zaidi ya watu milioni mbili.

XS
SM
MD
LG