Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:22

Kim Jong Il kiongozi wa Korea Kaskazini afariki


KIongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Il
KIongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Il

Televisheni ya taifa ya Korea ya Kaskazini imetangaza kwamba kiongozi mkuu Kim Jong Il amefariki kutokana na kuchoka kimwili na kiakili.

Shirika rasmi la habari la Korea kaskazini lilitangaza Jumatatu kwamba kiongozi huyo wa muda mrefu, aliyependa kujitenga na dunia, alifariki Jumamosi kutokana na mshtuko wa moyo alipokua anasafiri kwa treni kutoka moja wapo ya ziara yake ya mashambani.

KCNA imesema maziko yake yatafanyika Disemba 28 mjini Pyongyang, na kipindi cha maombolezi ya kitaifa kimetangazwa kuanzia Disemba 17 hadi 29.

Kim Jong Il alichukua madaraka mwaka 1994 baada ya kifo cha babake Kim Il Sung, Hakuna habari za kutosha, za kuaminika juu ya maisha ya Kim. Ilikua nadra kuonekana kwake hadharana na hata sauti yake haikusikika sana wakati wa uwongozi wake.

Atakumbukwa zaidi kwa kukaidi jumuia ya kimataifa katika kuimarisha mpango wa nuklia wa Korea ya Kaskazini wakati mamilioni ya wananchi wake wanakabiliwa na njaa.

Mwishoni mwa mwaka jana Bw. Kim alimpandisha cheo mwanawe mdogo wa kiume Kim Jong Un, kuwa Jenerali, katika kile kilichoonekana juhudi za kuongeza muda wa utawala wa familia moja wa taifa la kikomunisti kwa kizazi cha tatu.

Shirika la habari la taifa limewataka wananchi kumunga mkono Kim Jong Un kijana anaeaminika kua na umri wa miaka 28.

XS
SM
MD
LG