Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:18

Kim Davis aanza kazi baada ya kutolewa jela


Kim Davis (C) na mwanae Nathan Davis wakizungukwa na mapolisi wa kaunti ya Rowan, alipozungumza na vyombo vya habari huko Kentucky, Sept. 14, 2015.
Kim Davis (C) na mwanae Nathan Davis wakizungukwa na mapolisi wa kaunti ya Rowan, alipozungumza na vyombo vya habari huko Kentucky, Sept. 14, 2015.

Mfanyakazi wa mahakama moja nchini Marekani, ambaye alifungwa kwa kukataa kutoa leseni za ndoa kwa mashoga, alirudi kazini Jumatatu akisema hatamzuia naibu wake kutoa leseni hizo, lakini anahoji uhalali wa nyaraka hizo bila ya idhini yake.

Saa kadhaa baada ya Kim Davis kuwasili kwenye jengo la mahakama ya kaunti ya Rowan huko Kentucky, naibu wake Brian Mason alitoa leseni ya ndoa kwa mashoga, Shannon Wampler na Carmen Collins. Bibi.Davis alirejea kazini baada ya kuwa jela kwa siku tano.

Jaji mmoja wa mahakama ya serikali kuu alimhukumu kwa kukaidi amri yake ya kutoa leseni kwa mujibu wa uamuzi uliopitishwa na mahakama kuu ya Marekani hapo mwezi Juni kwamba mashoga wana haki ya kikatiba ya kuoana. Davis, mkristo mwenye imani kali alisema ndoa za jinsia moja zinakiuka imani yake ya dini. Amekuwa shujaa kwa baadhi ya wakristo wa-conservative nchini Marekani kwa kukataa kwake kutoa leseni kwa ndoa za watu wa jinsia moja.

Kim Davis na Mike Huckabee (L) mgombea urais wa Republican, Sept. 8, 2015.
Kim Davis na Mike Huckabee (L) mgombea urais wa Republican, Sept. 8, 2015.

Mfanyakazi huyo alisoma kutoka taarifa iliyoandikwa kwa mkono wakati ofisi yake ilipofunguliwa kuanza kazi, akisema “sitaki kuwa na mgogoro huu”. Sitaki kuwa kielelezo. Na kwa hakika sitaki kuadhibiwa.

Bibi. Davis alisema “yeye siyo shujaa ni mtu ambaye amebadilishwa kwa neema ya mwenyenzi mungu, ambaye anataka kufanya kazi, kuwa na familia yangu. Ninataka kuwahudumia majirani zangu kimya bila kukiuka imani yangu”.

Mason alitoa leseni za ndoa kwa mashoga wasiopungua saba wakati Bibi Davis alipokuwa hayupo kazini wiki iliyopita na kabla ya mashoga wa kwanza hapo Jumatatu kuomba leseni ya kufunga ndoa, alisema ataendelea kufanya hivyo.

XS
SM
MD
LG