Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:22

Khartoum yatangaza Sudan kusini ni adui.


Mwanajeshi wa Sudan akifanya doria kufuatia mapambano yao na kusini katika mji wa Talodi kilometa 50 kutoka eneo lililo na mzozo na kusini .
Mwanajeshi wa Sudan akifanya doria kufuatia mapambano yao na kusini katika mji wa Talodi kilometa 50 kutoka eneo lililo na mzozo na kusini .

Sudan Kusini na sudan zipo katika hali ya kivita aeleza mwanachama maarufu wa chama tawala.

Bunge la Sudan limetangaza kuwa Sudan Kusini ni adui kati kati ya ghasia zinazosambaa kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.

Baada ya upigaji kura mjini Khartoum jumatatu, waziri wa habari wa Sudan Kusini Barnaba Marial aliupinga uamuzi huo na kusema nchi yake si adui wa Sudan.

Rabi Abdelati Obeid mwanachama maarufu wa chama kinachotawala Sudan cha National Congress aliiambia Sauti ya Amerika kuwa hali kati ya nchi hizo mbili hivi sasa ni hali ya kivita.

Alisema Sudan Kusini haiheshimu mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini.

XS
SM
MD
LG