Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 12:52

Kesi ya Kenyatta ni Novemba huko ICC


Rais wa kenya, Uhuru Kenyatta (L) na Naibu Makamu Rais wake William Ruto wote wanakabiliwa na mashtaka huko ICC
Rais wa kenya, Uhuru Kenyatta (L) na Naibu Makamu Rais wake William Ruto wote wanakabiliwa na mashtaka huko ICC
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu - ICC - inasema kesi ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta sasa itasikilizwa Novemba 12. Mahakama ilitangaza alhamis tarehe mpya ya kuanza kwa kesi, baada ya kukubali ombi la timu ya utetezi ya Bwana Kenyatta ya kutaka muda zaidi wa kujiandaa kwa kesi yao.

Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa mwezi Julai, lakini mahakama ilisema kulikuwa na ucheleweshwaji katika uwasilishaji ushahidi. Bwana Kenyatta anashtakiwa kwa makosa matano ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa shutuma za kuhusika kwake katika kuchochea ghasia za kikabila ambazo zilitokea Kenya nzima baada ya uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2007. Zaidi ya watu 1,100 walikufa.

Naibu Makamu Rais, William Ruto na mkurugenzi wa kituo kimoja cha redio nchini Kenya, Joshua Arap Sang pia wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya ICC. Kesi yao imepangwa kusikilizwa septemba 10. Mahakama ilisema mwanzoni mwa mwezi huu taratibu zote huwenda zikafanyika nchini Kenya au Tanzania badala ya makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu iliyopo The Hague.

Wote watatu wanakana mashtaka yaliyotolewa dhidi yao. Licha ya kesi kuendelea kuwa wazi, Bwana Kenyatta alishinda mzunguko wa kwanza wa uchaguzi mkuu wa urais uliofanyika mwezi Machi pamoja na mgombea mwenza wake William Ruto.
XS
SM
MD
LG