Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:09

Kesi dhidi ya Ghailani yaendelea mjini New York.


Mtuhumiwa gaidi Ahmed Ghailani akiwa mahakamani.
Mtuhumiwa gaidi Ahmed Ghailani akiwa mahakamani.

Kesi dhidi ya Ahmed Khalfan Ghailani anayetuhumiwa katika mashambulizi ya mabomu katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka wa 1998 iliingia siku yake ya tatu Alhamis Mjini New York.

Waendesha mashitaka na mawakili wa utetezi waliwahoji mashahidi watatu kuhusiana na uhalifu anaodaiwa kufanya Ahmed Ghailani. Ghailani ambaye ni raia wa Tanzania, ni mfungwa wa kwanza katika gereza la Guantanamo Bay, nchini Cuba kufikishwa mbele ya mahakama ya wahalifu ya Marekani. Anakabiliwa na mashitaka 224 ya mauaji.

Miongoni mwa mashahidi waliohojiwa ni mtaalam wa vifaa vya ulipuaji kutoka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai FBI na mfanyibiashara raia wa Tanzania ambaye waendesha mashitaka wanasema alimuuzia Ghailani gari alilotumia kuhifadhia vilipuaji alivyotumia baadaye kulipua ubalozi wa Marekani mjini Dar-es-Salaam. Mfanyibiashara huyo sio mtuhumiwa katika kesi hiyo.

Mamia ya mashahidi wanatazamiwa kutoa ushahidi wao wakati wa kesi hii ambayo inatazamiwa kuendelea kwa miezi mitatu hivi.

Jaji wa Marekani Lewis Kaplan amesema serikali haiwezi kukusanya habari za kijasusi kutoka kwa mfungwa na kisha kuzitumia habari hizo katika kesi ya uhalifu.

Tamko kutoka kwa mkuu wa sheria wa Marekani Eric Holder na baadaye kutoka kwa jaji Lewis yakiashiria kuwa Ghailani huenda akaendelea kuzuiliwa kisheria kama adui hata kama mahakama itamwachia, limezusha maswali kutoka kwa wasomi wanaohoji ikiwa ipo haja ya kuendelea na kesi hii.

XS
SM
MD
LG