Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:11

Kerry atembelea Nigeria


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (L) akizungumza na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan mjini Lagos Jan. 25, 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (L) akizungumza na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan mjini Lagos Jan. 25, 2015.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry anasema marekani itaendelea kulisaidia jeshi la Nigeria katika mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram.

Bwana Kerry ambaye aliwasili jumapili katika mji mkuu wa Nigeria, Lagos alizungumza muda mfupi baada ya wanajeshi wa Nigeria kuzima shambulizi moja lililofanywa na wanamgambo wa Boko Haram nje ya mji mkuu Maiduguri katika jimbo la Borno.

“sababu ya msingi ambayo Rais wa Marekani, Barack Obama aliniomba nije hapa wakati huu ni kusisitiza kwa wa-Nigeria wote azma ya Marekani kuweza kushirikiana nanyi hata zaidi ya hapa katika juhudi za kulirudisha nyuma kundi la Boko Haram au ghasia nyingine zozote za kundi la wenye msimamo mkali”.

John Kerry
John Kerry

Bwana Kerry alikutana na wagombea wawili wa urais wanaoongoza nchini humo, Rais aliyeko madarakani Goodluck Jonathan na mgombea mkuu wa upinzani Muhammadu Buhari kabla ya uchaguzi wa urais nchini humo February 14.

Waziri Kerry alisema “ni muhimu sana’ uchaguzi kufanyika kwa amani, wenye hadhi, uwazi na uwajibikaji akiongeza kuwa mtu yeyote anayesababisha ghasia za uchaguzi hatokaribishwa nchini Marekani. “mtu yeyote anayeshiriki katika mipango au kutoa wito wa kusambaza ghasia dhidi ya raia lazima awajibishwe ikiwemo kunyimwa visa ya Marekani. Ghasia hazina nafasi katika uchaguzi wa kidemokrasia na ninawahakikishia kwamba watakaofanya ghasia hizo hawatakaribishwa nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG