Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:13

Kenya yasisitiza kufunga kambi ya Daadab


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Somalia, March 7, 2017.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Somalia, March 7, 2017.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameendelea kusisitiza kuwa bado msimamo wa serikali yake ni kuifunga kambi ya wakimbizi ya Daadab.

Kenyatta amesema haya wakati alipokutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini humo licha ya jitihada za mashirika ya kibinadamu kuishtumu serikali kwa uamuzi wake wa kufunga kambi hiyo ya Daadab.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA amesema hili limekuja takriban mwezi mmoja baada ya Mahakama moja jijini Nairobi kuamuru kuwa mpango wa serikali ya Kenya kufunga kambi ya Daadab na kuwarejesha makwao wakimbizi ni kinyume cha sheria.

Amesema alipofika zamu yake ya kuzungumza na wandishi wa habari Bwana Antonio Guterres alionekana kukwepa suala hilo.

Lakini ameleza kufurahishwa na Kenya kwa juhudi zake za kujitolea na kuimarisha usalama katika Afrika Mashariki na Kati na Afrika kwa ujumla hususan nchini Somalia na Sudan Kusini.

Katika ziara ambayo ilionekana na wengi kuwa nafasi bora ya kuendeleza uhusiano bora kati ya Umoja wa Mataifa na Kenya baada kushuhudiwa mgogoro kati ya Kenya na Katibu Mkuu wa Umoja huo aliyeondoka Ban Ki Moon kutokana na kumfuta Luteni Johnson Ondieki kutoka jeshi la Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini (UNMISS) mwaka jana.

Wakati huo huo Katibu Mkuu aliyeizuru pia Somalia ameeleza kuridhishwa na Kenya kwa ukarimu wake katika kushirikiana na Umoja wa Mataifa na atachukua hatua kurejesha fadhila hizo kwa taifa hilo.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa utazisaidia Kenya, Somalia, Sudan Kusini na Ethiopia kiwango cha dola bilioni kuzisaidia nchi hizi kukabiliana na hali ya ukame ambayo imewaathiri watu wengi katika maeneo hayo.

Baadaye Bwana Guterres alihudhuria mkutano wa kuadhimisha siku ya wanawake ulimwenguni hapa jijini Nairobi na kusisitiza kuwa wanawake waheshimiwe na kupatiwa fursa za uongozi.

XS
SM
MD
LG