Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:11

Ziara za rais Kenyatta nje za zuwa utata


Rais Kenyatta akiwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa 2015 (COP21) at Le Bourget, karibu na Paris, France, November 30, 2015.
Rais Kenyatta akiwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa 2015 (COP21) at Le Bourget, karibu na Paris, France, November 30, 2015.

Kulingana na wanasiasa wa upinzani,kwa kawaida Rais Kenyatta anaandamana na kundi kubwa la wanasiasa na maafisa wa serikali wasiokua na umuhimu au mchango wowote kwenye ziara hizo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:50 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Ziara za mara kwa mara za Rais Uhuru Kenyatta katika nchi za nje zinaendela kuzua hisia tofauti nchini Kenya,huku wapinzani wa serikali wakidai ujumbe mkubwa wa rais kwenye ziara hizo unavuja pesa za serikali na hauna manufaa yoyote kwa taifa.

Tangu kuchukua hatamu ya uongozi karibu miaka miwili iliyopita,Rais Kenyatta amefanya ziara 43 za mataifa ya nje ukilinganisha na Rais Kibaki aliyefanya ziara 30 katika muda wa miaka 10 ya utawala wake.

Katika muda wa wiki moja tu iliyopita,Rais Kenyatta alikwenda nchini Malta kuhudhuria mkutano wa jumuiya ya Madola,baadaye alikwenda Paris kwa mkutano wa Madola na kabla ya mwisho mwa wiki alikwenda Afrika Kusini kukutana na viongozi wa Uchina.

Hata hivyo watalaamu wa maswala ya Diplomasia wanadai ziara hizo ni muhimu kwa sababu Rais Kenyatta ndiye Balozi wa kwanza wa nchi hii akifuatiwa na waziri wake wa mashauri ya nchi za nje.

Kwa hivi sasa,Rais Kenyatta anatakia kupunguza ziara zake katika nchini za nje na wakati huo kuwachuja maafisa aliokokwenye msafara wake.

XS
SM
MD
LG