Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:59

Mradi wakuzuia na kudhibiti magonjwa wazinduliwa Kenya


wafanyakazi wa afya wakiwa wamevaa mavazi ya kinga kutokana na magonjwa ya kuambukizwa.
wafanyakazi wa afya wakiwa wamevaa mavazi ya kinga kutokana na magonjwa ya kuambukizwa.

Tangu mwaka 2014 Afrika Magharibu, ilishuhudia mlipuko mkubwa zaidi wa Ebola katika historia, ulouwa zaidi ya watu elfu 11, na kusababisha watu kuanza kufikiria juu ya kitisho cha kutokea milipuko ya ugonjwa duniani. Virusi vya Ebola sio pekee vinavyosababisha ugonjwa kutoka wanyama hadi binadamu , na wakati idadi ya watu inaongezeka duniani na mahitaji ya chakula kuzidi vitisho Zaidi vinajitokeza.

Kwenye hoteli moja mjini Nairobi siku ya Jumanne , idara ya kilimo na chakula ya Umoja Mataifa FAO, kwa pamoja na idara ya misaada ya kimataifa ya Marekani USAID, zilizindua kitengo cha Afrika Mashariki cha mradi wa FAO cha vitisho vya majanga ya ugonjwa, EPT-2. Mradi huo unakusudiwa kutambuwa, kuzuia na kudhibiti magonjwa mapya yanayosababishwa na virusi vinavyotoka kwa wanyama na kuwaambukiza binadam.

Subhash Morzaria ni mratibu wa kimataifa wa mradi wa EPT-2 katika idara ya FAO.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:04 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Anasema magonjwa haya yanaweza kuambukizwa kupitia hewa au kushika majimaji ya mwili au kitu kingine kile yaliyoathiriwa.

Bw. Morzaria anasema, vyovyote vile maambukizo yanavyotokea, cha muhimu hapa ni vipi tunakabiliana na magonjwa haya yakiendelea miongoni mwa wanyama wetu, kwani hapo ndipo tuko hatarini kukabiliwa na majanga makubwa yanayosababisha vifo.

Ebola ni mojawapo tu ya magonjwa haya kutoka wanyama. Mengine ni pamoja na HIV na ukimwi, homa ya mafua hususan zile zijulikanao kama homa ya ndege homa ya nguruwe na kadhalika.

Kulingana na kituo cha Marekani cha kuzuia na kudhibiti magonjwa CDC, takriban sita kati ya magonjwa 10 ya kuambukizwa katika binadamu yanasamba kutoka wanyama.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa idadi ya watu duniani iliyo takriban billioni 7.3 sasa, itapanda na kufikia watu billiono 9.9 ifikapo mwaka 2050. Ongezeko hili la haraka la idadi ya watu, inamaanisha kutakua na mahitaji makubwa ya chakula.

Bw. Morzaria anasema, sasa mifumo hii ya uzalishaji itabadilika haraka ili kukidhi mahitaji hayo, na inawezekana kwamba baadhi ya tabia za hatari ya kuzalisha wanyama zikajitokeza na hiyo tabia hizo za hatari zinaweza kubuni mazingira kukuza na kuenea kwa virusi vipya.

Mkurugenzi mwaandamizi wa idara za wanyama Kenya, Dr. Kisa Juma Ngeiywa, anaongeza kusema kwamba virusi vipya vinaweza kusambaa mbali zaidi kutokana na jamii ya leo inayosafiri safiri.

Hata hivyo Bw. Morzaria anasema, kila mtu ni kitisho. virusi havichaguwi baina ya masikini au tajiri. Inakwenda na kuambukiza mtu, na kuwauwa watu ikiwa ni virusi vya hatari.Kwa hivyo hili ni tatizo linalotia wasiwasi dunia mzima.

Hapo mwezi October, USAID ilitangaza ufadhili mpya wa takriban dola millioni 87 kwa ajili ya mradi huo. Fedha hizo zitatumika kusaidia seriklai na idara za wanyama, kufahamu vyema zaidi mifumo ya wanyama, ikiwa ni pamoja na hatari ya kusamba kwa haraka na kusaidia kufanya ufuatiliaji wa mapema, kadhalika kutambuwa virusi vinoweza kujitokeza.

XS
SM
MD
LG