Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:16

Majeshi ya Kenya hatimaye yaingia Kismayu


Bandari ya Kismayo, Somalia
Bandari ya Kismayo, Somalia

Habari nyingine zinasema majeshi ya Kenya yanashikilia zaidi eneo la kaskazini mwa mji huo ambako kuna barabara ya kwenda Mogadishu

Jeshi la Kenya linasema majeshi yake yameingia kwenye mji wa Kismayo nchini Somalia katika operesheni ya kuuchukua tena mji huo kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabab wenye uhusiano na al-Qaida.

Msemaji wa jeshi la Kenya, Kanali Cyrus Oguna anasema shambulizi la mapema Ijumaa lilijumuisha majeshi yote ya majini na ya anga yakishirikiana na wanajeshi wa Umoja wa Afrika na ya serikali ya Somalia.

Oguna alisema mji huo ulitekwa "bila upinzani mkubwa", hata hivyo mashahidi na majeshi ya al-Shabab wanasema mapigano yanaendelea ndani na kuzunguka mji huo.

Mwanzoni mwa wiki hii Kenya ilisema jeshi lake lilifanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo muhimu ya waasi huko Kismayo. Wanamgambo wa al-Shabab wanatumia bandari ya mji huo kuingiza silaha na vifaa vingine ili kuwasaidia waasi wenzao kupambana dhidi ya serikali.

Kundi hilo la uasi linataka kuweka utumiaji wa sheria kali ya ki-islam kote nchini Somalia. Kundi hilo liliwahi kudhibiti eneo la kusini na kati kati mwa Somalia, lakini limepoteza mamlaka yake yote na kwenda kwa majeshi yanayounga mkono serikali tangu yalipofanya shambulizi moja kubwa la kujilinda mwaka jana.
XS
SM
MD
LG