Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:48

Odinga akanusha lawama za washukiwa wa the Hague


Raila Odinga, Waziri Mkuu wa Kenya
Raila Odinga, Waziri Mkuu wa Kenya

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amekanusha kuhusika na shinikizo la kuwapeleka the Hague washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita nchini humo. Bwana Odinga alisema hayo katika hotuba yake kwa taifa Jumatano siku moja kabla ya baadhi ya watuhumiwa hao kutokea mbele ya mahakama ya ICC huko the Hague hapo Alhamisi.

Washukiwa sita wakiwemo washirika wa karibu wa Raila Odinga wamekwenda the Hague kuhudhuria vikao vya mwanzo vya madai yanayowakabili ambavyo vitaamua endapo watakuwa na kesi ya kujibu ama la kuhusiana na kushiriki kwao katika ghasia zilizopelekea vifo vya zaidi ya watu 1,000 na wengine wengi kukoseshwa makazi.

Mwendesha mashtaka mkuu ICC, Louis Moreno-Ocampo, alifanya safari kadhaa nchini Kenya na kukutana na watu mbali mbali ili kuweza kupata ushahidi wa kile kilichotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 nchini humo.

Hatua hii imepelekea kuwepo mtazamo tofauti wa kisiasa nchini Kenya, baina ya chama tawala kinachoongozwa na Rais Mwai Kibaki na chama kikuu cha upinzani cha Waziri Mkuu Raila Odinga.

XS
SM
MD
LG