Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:54

Raia wa Kenya hawajazuiwa kuingia Marekani


Rais wa Marekani, Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald Trump

Raia wa Kenya hawatoathiriwa na amri ya kiutendaji ya muda iliyosainiwa na Rais Donald Trump inayozuia raia wa kigeni kutoka nchi saba za kiislamu kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa tovuti ya Ubalozi wa Marekani nchini Kenya raia wa Kenya hawajazuiliwa kuingia Marekani wakati taratibu za kuchunguzwa wahamiaji zikiendelea kupitiwa.

Nchi ambazo zimetajwa katika amri hiyo ya kiutendaji ni Somalia, Yemen, Sudan, Iraq, Iran, Syria na Libya.

Ubalozi umesema habari zilizoenea na taarifa zinazotolewa na mitandao ya kijamii zikidai kuwa raia wa Kenya wamezuiliwa kuingia Marekani hazina ukweli hata kidogo.

Taarifa ya ubalozi imesema amri hii haitabadilisha makubaliano ya usawa wa utoaji viza baina ya nchi mbili au uhalali wa wasafiri kuingia Marekani kwa hali yeyote.

Wakati huo huo ubalozi wa Marekani mjini Nairobi unaendelea kutoa viza ya miaka mitano ya kuingia na kutoka kwa Wakenya wanaotaka kwenda Marekani kwa ajili ya utalii, biashara, kusoma, na tunaendelea kushughulikia viza za uhamiaji (green cards) kwa Wakenya.

Hakuna kiwango kwa idadi ya Wakenya wanaoruhusiwa kuchukua viza au kuingia Marekani.

Kadhalika amri hii haitaathiri muda alioruhusiwa mgeni kutoka Kenya kukaa Marekani, kawaida ni miezi sita kwa watalii, kitu ambacho kinaamuliwa wakati wakifika uhamiaji katika sehemu wanayoteremka kutoka kwenye ndege.

“Tutaendelea kuwapokea wasafiri halali wa Kenya nchini Marekani na tutatangaza mabadiliko yeyote yatakayo waathiri wasafiri wanaokwenda Marekani katika tovuti zetu (travel.state.gov, https://travel.state.gov/content/visas/en.html, https://ais.usvisa-info.com/en-ke/iv andhttps://ais.usvisa-info.com/en-ke/niv).

XS
SM
MD
LG