Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:24

Wanasiasa Kenya washtakiwa kwa 'kuchochea chuki'


Wanasiasa wanane nchini Kenya walipofikishwa mbele ya mahakama moja mjini Nairobi siku ya Ijumaa na kufunguliwa mashtaka ya kuchochea vurugu na chuki. Washukiwa hao walikuwa wameshikiliwa katika vituo mbali mbali vya polisi tangu siku ya Junmanne.
Wanasiasa wanane nchini Kenya walipofikishwa mbele ya mahakama moja mjini Nairobi siku ya Ijumaa na kufunguliwa mashtaka ya kuchochea vurugu na chuki. Washukiwa hao walikuwa wameshikiliwa katika vituo mbali mbali vya polisi tangu siku ya Junmanne.

Na BMJ Muriithi

Wanasiasa wanane nchini Kenya walifikishwa mbele ya mahakama moja mjini Nairobi siku ya Ijumaa na kufunguliwa mashtaka ya kuchochea vurugu.

Washukiwa hao, ambao walikuwa wamezuiliwa katika vituo mbali mbali vya polisi tangu siku ya Jumanne, walikanusha mashtaka hayo kupitia mawakili wao ambao waliandamana nao mahakamani.

Watuhumiwa hao, wanaotoka mirengo yote milwili ya kisiasa - yaani CORD na JUBILEE- ni Seneta wa Machakos, Johnson Muthama, wabunge Timothy Bosire (Kitutru Masaba), Junet Mohamed (Suna Mashariki) Aisha Jumwa (Mwakilishi wa wanawake wa Kilifi) na Florence Mutua (Busia).

Wengine walikuwa ni Ferdinad Waititu (Kabete), Moses Kuria (Gatundu) na Kimani Ngunjiri (Bahati).

Nje ya Mahakama ya Milimani, mjini Nairobi
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:48 0:00

Upande wa mashtaka ulisema kuwa kwa tarehe tofauti katika maeneo mbali mbali, wanasiasa hao walitoa matamshi wa kuchochea chuki, kinyume cha sheria za Kenya.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika nchini Kenya, Kennedy Wandera, alisema siku ya Ijumaa kuwa watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani mwendo wa saa kumi na moja na dakika arobaine na tano asubuhi huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.

“Polisi wamesema waliwafikisha kortini mapema hivyo kabla ya wakaazi wengi wa Nairobi kuamka kwa sababu walitaka kupuunguza uwezekano wa baadhi ya wafuasi wa wanasiasa hao kuanza kufanya maandamano ya barabarani kama ambavyo wamekuwa wakifanya tangu siku ya Jumanne kila wanapowaona viongiozi wao wakisafirishwa,” alisema Wandera.

Kenya Milimani
Kenya Milimani

Baada ya kusomewa mashtaka, upande wa mashtaka ulipinga vikali ombi la mawakili kwamba washtakiwa hao waachiliwe kwa dhamana.

Kulikuwa na hali ya wasiwasi mahakamani pale mmoja wa watuhumiwa, Mbunge wa Bahati, Kimani Ngunjiri, alipozirai akiwa kizimbani, na kubidi hakimu kuhairisha kikao kwa muda mfupi ili kuwapa nafasi watabibu kumhudumia.

Mawakili James Orengo na Okongo Omgeni walilalamika kuwa wateja wao wameteseka sana tangu mahakama hiyo kuamuru kuwa wawekwe kizuizini kwa muda wa siku ili kuwapa wachunguzi muda wa kutosha.

Lakini viongozi wa mashtaka Leonard Maingi na Daniel Kirori walipinga kuachiliwa kwa dhamana na kusema makosa waliyoshtakiwa nayo ni makubwa mno.

“Hatuongei kuhusu wizi mdogo mdogo hapa. Huu ni uhalifu mkubwa na washukiwa huenda wakarudia makosa hayo endapo wataachiliwa kwa dhamana,” Gazeti la ‘The Star’ lilinukuu taarifa ya upande wa mashtaka.

Ombi la kutaka washukiwa hao kuachiliwa kwa dhamana lilijadiliwa siku nzima Ijumaa.

Maafisa wa polisi waliokuwa wamejihami walionekana wakilnda doria nje ya mahakama ya Milimani, huku magari yao yakizunguka eneo lote linalizingira korti hilo. Wanasiasa, familia za washukiwa na wafuasi wao waliopnekana nje na ndani ya mahakama hiyo kutka asubuhi hadi jioni.

“Tunataka waachiliwe kwa dhamana kwa sabau iwapo watafungiwa tena, wtakuwa kwa rumbnde ya polisi tena hadi Jumatatu. Unavyojua ni kwamba wengine wao tayari wamegonjeka,” mke wa mmoja wa washukiwa alinukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema.

Wakati huo huo, tume ya haki na Maridhiano ilipinga vikali kuachiliwa kwa washtakiwa hao kwa dhamana.

XS
SM
MD
LG