Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:33

Uchunguzi waanza kutokana na kuchomwa kanisa la kihistoria Marekani


Mtumishi wa idara ya upelelezi ya jimbo la Mississipi akitoa baadhi ya ushahidi kutoka eneo la tukio.
Mtumishi wa idara ya upelelezi ya jimbo la Mississipi akitoa baadhi ya ushahidi kutoka eneo la tukio.

Maafisa wa usalama wa Marekani wameanzisha uchunguzi wa haki za kiraia baada ya kanisa moja la watu weusi katika jimbo la kusini la Mississipi baada ya kuchomwa moto na kuandikwa kwa rangi alama ya “Mpigie kura Trump” .

Kanisa hilo la kihistoria lililojengwa miaka 111 iliyopita la Hopewell Missionary huko Greenville Mississipi liliharibika sana kutokana na maji mengi ya kuzima moto na moshi hapo Jumanne usiku.

Meya wa Greenville Errick Simmons alisema kwamba wanalichukulia tukio hilo kama uhalifu wa chuki kwasababu ya ujumbe wa kisiasa ambao wanaamini ulikuwa na lengo la kusababisha kitisho kwsa waumini wapiga kura.

Anasema kitendo hicho ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya haki ya wananchi kuabudu kwa uhuru.

Meya huyo alisema kwamba Idara ya upelelezi wa jinai , FBI na idara ya upelelezi ya jimbo la Mississipi wanasaidia katika uchunguzi huo.

XS
SM
MD
LG