Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:40

Tetemeko la ardhi lazuka tena Kagera


Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Tetemeko la ardhi limetokea tena mkoani Kagera nchini Tanzania na kusababisha hofu kwa wananchi.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini hofu hiyo inatokana na tetemeko lenye ukubwa wa 5.7 kwa vipimo vya Richter lililotokea mwaka jana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10 na kujeruhi watu wasiopungua 200 na kuwaacha mamia bila makazi.

Wananchi waliozungumza na gazeti hilo, katika Manispaa ya Bukoba, wilaya za Missenyi, Muleba na Karagwe wamesema tetemeko hilo lilitokea saa saba usiku wa kuamkia Jumapili.

Wananchi hao wamesema kuwa baadhi ya wakazi wa mjini Bukoba walilazimika kulala nje ya nyumba zao kutokana na kishindo cha tetemeko hilo.

XS
SM
MD
LG