Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 13:09

Kabila akabiliwa na upinzani kuzungumza na M23.


Wapiganaji wa M23 wawasili Goma
Wapiganaji wa M23 wawasili Goma
Serikali ya Rais Joseph Kabila imetangaza mpango wa kuanza mazungumzo na waasi wa kundi la M23 ili kutafakari na kukagua mkataba wa amani wa Marchi 2009 baina ya Serikali na waasi.

Mkutano huo utakaofanyika mjini Kampala unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe wa serikali, waasi wa M23 pamoja na wajumbe wa mashirika ya kiraia. Hata hivyo ajenda rasmi ya mkutano huo bado haijatangazwa.

Kwa siku mbili mfululizo Rais Kabila amekuwa akikutana na baadhi ya viongozi wa idara za serikali na wabunge ilikuwapa mtizamo wake kuhusu vita vya Kivu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:52 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Aubin Minaku, Spika wa bunge la DRC na mshirika wa karibu wa Rais Kabila, akizungumza na vyombo vya habari amesema kwamba mkutano huo wa Kampala unalenga kutafakari juu ya malalamiko ya waasi wa M23.

Kauli hiyo ya spika wa bunge imefuatia ombi la waasi wa M23 la kutaka upinzani wa kisiasa, mashirika ya kiraia na wakongomani wanaoishi nje ya nchi kushirikishwa kwenye mazungumzo. Spika wa bunge la DRC amesema kwamba siyo vibaya kuweko na watu wa tabaka zote za taifa kushirikishwa kwenye mazungumzo.

Suala la kuwepo kwa mazungumzo na waasi limezusha utata mkubwa huko kinshasa ambapo vyama vikuu vya upinzani vinapinga mazunguzmo hayo. Msemaji wa chama kikuu cha upinzani UDPS, Augustin Kabuya ameiambia VOA kwamba hawatoshiriki katika aina yeyote ile ya mazungumzo baina ya serikali na waasi wa M23.

UDPS inaeleza kwamba serikali ya Kabila, si halali sawa na vile waasi wa M23, na kuwataka waasi hao kutotumia jina la kiongozi wao, Etienne Tshisekedi katika kutetea vita vyao, kwa sababu UDPS haiwezi kamwe kutumia silaha ilikuchukuwa madaraka.

Lakini kwa upande wake chama cha UNC cha Vital Kamerhe kimesema kwamba kiko tayari kuhudhuria mazungumzo ya Kampala ikiwa kitaalikwa.

Msemaji wa tawi la kisiasa wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa ambaye ameiambia VOA kwa njia ya simu kwamba wamepokea mualiko wa kwenda Kampala kwa ajili ya mazungumzo, amesisitiza kwamba ajenda ya mkutano huo ni lazima iwape nafasi wapinzani na mashirika ya kiraia kuhudhuria mkutano huo.

Makundi mengine ya wapiganaji pia yameelezea nia yao ya kutaka yashirikishwe kwenye mazungumzo sawa na M23.
XS
SM
MD
LG