Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:07

John Kerry ateuliwa kuchukua nafasi ya Clinton


Seneta John Kerry ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Hillary Clinton wote kutoka chama cha Democrat
Seneta John Kerry ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Hillary Clinton wote kutoka chama cha Democrat
Maafisa waandamizi wa Marekani wanasema Rais Barack Obama atamteuwa seneta John Kerry kuchukua nafasi ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Maafisa wa utawala wanasema bwana Obama atatangaza rasmi uteuzi huo baadae Ijumaa.

Kerry, m-Democrat kutoka jimbo la kaskazini mashariki la Massachusetts amehudumu kama mwenyekiti wa kamati ya seneti inayoshughulika na uhusiano wa nje na amesafiri kwenda sehemu mbali kwa niaba ya Rais Obama kujadili masuala muhimu duniani kote kutoka Afrika hadi Pakistan. Pia anatambulika kama mkongwe wa vita vya Vietnam.

Kerry mwenye umri wa miaka 69 aliwahi kuwania nafasi ya urais katika chama cha Democrat mwaka 2004 na kushindwa kinyang’anyiro hicho na Rais aliyekuwa madarakani wakati huo George W.Bush.Kama akipitishwa na seneti, Kerry atachukua nafasi ya hivi sasa ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton ambaye alitangaza hana mpango wa kuendelea katika wadhifa huo katika muhula wa pili wa utawala wa Obama.
XS
SM
MD
LG