Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:34

Jeshi laahidi kukabidhi madaraka kwa mshindi Misri.


Mgombea wa Muslim Brotherhood Mohamed Morsi akizungumza na waandishi wa habari.
Mgombea wa Muslim Brotherhood Mohamed Morsi akizungumza na waandishi wa habari.

Chama cha Muslim Botherhood chadai kinaongoza katika kura ya duru ya pili.

Viongozi wa kijeshi wa Misri wameapa kuheshimu ahadi yao ya kukabidhi madaraka kwa rais mpya atakayechaguliwa ifikapo mwishoni mwa mwezi.

Tangazo la utawala huo wa kijeshi Jumatatu limekuja baada ya wao kutangaza katiba mpya ya muda, hatua ambayo inapunguza nguvu ya mshindi wa uchaguzi atakayepatikana. Baraza hilo la kijeshi limeongoza nchi hiyo tangu Machi 2011.

Wakati huo huo mgombea wa Muslim Brotherhood Mohamed Morsi alijitangazia ushindi katika uchaguzi huo ambao ni wa kwanza wa rais baada ya uasi nchini humo.

Chama cha Muslim Brotherhood kimesema matokeo yasiyo rasmi yanaonyesha alishinda asilimia 52 ya kura katika uchaguzi wa siku mbili wa duru ya pili ambao ulimalizika Jumapili. Chama cha Brotherhood kimesema madai yake ya ushindi yanatokana na matokeo yaliohesabiwa na wawakilishi wa chama hicho katika karibu kila kituo cha kupigia kura nchini humo.

XS
SM
MD
LG