Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:18

Japan yakumbuka waathiriwa wa tetemeko la ardhi mwaka jana


moja ya jengo lililoharibiwa na tsunami katika mji wa Ishinomaki, Machi 9, 2012.
moja ya jengo lililoharibiwa na tsunami katika mji wa Ishinomaki, Machi 9, 2012.

maelfu ya watu wajitokeza maeneo mbalimbali kukumbuka walioathiriwa na tetemeko la ardhi mwaka jana.

Jumapili ilikuwa siku ya maadhimisho ya tetemeko kubwa la ardhi lililoathiri zaidi ya watu elfu 20 huko Japan wakiwemo waliokufa na majeruhi.

Tetemeko la ukubwa wa kipimo cha Rikta 9.0 lilipiga japan Machi 11 majira ya saa tisa mchana na kufanya uharibu mkubwa wa nyumba za watu na majengo mbalimbali nchini humo.

Jumapili katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo watu walijitokeza kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea tetemeko hilo la ardhi.

Hotuba mbalimbali zilitolewa zikiongozwa na waziri mkuu wa nchi hiyo pamoja na uwekaji wa mashada ya maua katika maeneo ya tukio hilo.

Watu walioshuhudia matukio ya leo wanasema ilikuwa hali ya kusisimua pale ilipotimu majira ya saa nane mchana ambapo tetemeko hilo ndipo lilipiga mwaka jana, watu wote walinyamaza kimya kuheshimu na kukumbuka waliokufa na kuathiriwa katika janga hilo.

XS
SM
MD
LG