Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:43

Jamhuri ya Afrika ya Kati kujadiliana na waasi


Wanajeshi wa nchi za Afrika ya Kati (FOMAC) wakiwasili katika uwanja wa ndege mjini Bangui, December 31, 2012.
Wanajeshi wa nchi za Afrika ya Kati (FOMAC) wakiwasili katika uwanja wa ndege mjini Bangui, December 31, 2012.
SerikaliSerikali ya jamhuri ya Afrika ya Kati na kundi mseto la waasi nchini humo Seleka yaripotiwa wanakaribia kufanya mazungumzo ya amani wiki ijayo kufuatia juhudi za upatanishi kutoka kwa viongozi wa kikanda. Kundi la wanajeshi wa nchi za Afrika ya Kati liliweka udhibiti nje ya mji mkuu Bangui Jumatano, na kuonya wote , serikali na waasi kuwa uhasama zaidi baina yao hutavumiliwa.

Takriban wanajeshi mia tano wa nchi za Afrika ya Kati waliendelea kufanya doria nje ya mji wa Damara na kuweka eneo lisiloruhusiwa wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wala wapiganaji wa kundi mseto la waasi linalojiita Seleka, na ambalo limedhibiti thuluthi moja ya nchi katika muda wa wiki tatu zilizopita. Mkuu wa jeshi hilo la kikanda linalojulikana kama FOMAC jenerali Jean Felix Akaga alisema majeshi yake hayataachia mji wa Damara ulioko kilomita 75 tu kutoka mji mkuu Bangui.
Anasema ikiwa waaasi watashambulia mji wa Damara, itakuwa na maana wametangaza vita na kwamba wapo tayari kupigana kundi la majeshi ya kikanda kutoka nchi za Afrika ya Kati- FOMAC. Aidha Jenerali Akaga alisema majeshi ya FOMAC yanazuia majeshi ya serikali kuelekea kaskazini kupigana na wapiganaji wa kundi la Seleka. Alisema mji wa Damara ni tulivu na thabiti.

Hatua hiyo imechukuliwa ili kuwaleta pamoja wawakilishi wa serikali na viongozi wa Seleka katika majadiliano ya amani mjini Libreville, Gabon hapo Januari 10. Pande zote mbili zimesema zipo tayari kwa majadiliano.

Waasi wamekuwa mji wa Sibut, yapata kilomita 180 kutoka mji mkuu tangu Jumamosi. Na kwa mara nyingine wamesema wanasitisha hatua ya kuingia mji mkuu ili kutoa nafasi kwa majadiliano. Lakini katika siku za nyuma wamevunja ahadi zao wakisema kuwa wameshambuliwa na vikosi vya serikali.

Mji wa Damara Jumatano ulikuwa mtulivu, lakini kulikuwa na malori 32 yaliyojaa wanajeshi kutoka Chad wakiwa na silaha nzito. Wanajeshi hao ni sehemu ya wanajeshi wa kikanda FOMAC. Wengine wanatoka Jamhuri ya Congo na Gabon.

Watu wachache waliosalia huko Damara wanasema wana hofu kuu na kwamba wamezificha familia zao vichakani wakisubiri mzozo huo. Mkazi wa mji huo Andipassera Bertin anasema wamechoshwa na maasi. Anasema wake zao, watoto na jamaa zao wanataabika vichakani walipojificha. Anasema kuna baridi kali usiku na mbu wengi. Wakazi pia wanasema hospitali ya mji huo pamoja na soko zimefungwa na hawana namna ya kupata dawa wala chakula.

Kundi la Seleka ni mkusanyiko wa makundi manne ya waasi na yalianza mapigano dhidi ya serikali kati ya mwaka wa 2005 na 2006. Sasa wanadai serikali itekeleze kikamilifu mktaba iliyofikia pamoja nao mwaka wa 2007 na 2011 na wanamtaka rais Francois Bozize aondoke mamlakani. Waasi hao wanasema walitakulipwa fedha kwa kusalimisha silaha zao na kushirikishwa kwenye jeshi la kitaifa. Naye rais Bozize anasema yupo tayari kwa mazungumzo yasiyo na masharti kuunda serikali ya mseto.
XS
SM
MD
LG