Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 12:45

Operesheni ya kuchukua Mosul yaendelea

Mwanajeshi wa Iraq avalia bendera ya Iraq wakati vikosi vya Serikali vikikaribia kuuchukua tena Mji wa Mosul, Oktoba. 20, 2016.
Mwanajeshi wa Iraq avalia bendera ya Iraq wakati vikosi vya Serikali vikikaribia kuuchukua tena Mji wa Mosul, Oktoba. 20, 2016.

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider Al-Abadi, amesema kuwa operesheni ya kuuchukua tena mji wa Mosul, inaendelea haraka kuliko ilivyotarajiwa.

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider Al-Abadi, amesema kuwa operesheni ya kuuchukua tena mji wa Mosul, inaendelea haraka kuliko ilivyotarajiwa.

Al-Abadi ameyasema hayo mjini Paris,Ufaransa, ambako mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa ya Magharibi na yale ya Mashariki ya Kati, wamekuwa wakikutana kujadili mbinu za kurejesha utulivu na amani baada ya kundi la Islamic State kushindwa na kuondolewa mjini Mosul.

Jumatano, Jenerali Gary Volexy wa Marekani anayeongoza muungano wa kijeshi nchini Iraq ameomba vikosi vinavyopigana Mosul kufanya operesheni kwa taratibu ili maadui wasipate nafasi.

Gary Volexy, amewaambia waandishi wa habari kwa njia ya simu, kuwa anatarajia kwamba wapiganaji wa Islamic State watatumia mbinu za kawaida za vita, hadi pale watakaposhindwa mjini Mosul.

XS
SM
MD
LG