Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:10

Majeshi ya Iraq na wakurdi yakomboa vijiji kadhaa nje ya Mosul


Mapambano katika mji wa Mosul.
Mapambano katika mji wa Mosul.

Majeshi ya Iraq na wakurdi yamekomboa vijiji kadhaa nje ya mji wa kaskazini wa Mosul wakati wakiwa katika mapigano ya kutaka kukomboa udhibiti wa eneo hilo kutoka kwa kundi la Islamic State.

Operesheni iliyoungwa mkono na mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani na kuhusisha majeshi ya wasunni na washia yameingia siku ya pili Jumanne huku mapigano yakiendelea nje ya mji wa Mosul.

Rais wa wakurdi Masoud Barzani anasema siku ya kwanza ya mapigano imepelekea kukombolewa kwa kilometa 200 za mraba. Anasema Mosoul itakombolewa na kuongeza kwamba wapiganaji wake wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha mji huo hauharibiwi na vita kama ilivyo kwa mji wa Allepo Syria.

Hii ni operesheni kubwa kuliko zote tangu majeshi ya Marekani kuondoka miaka mitano iliyopita lakini wameelezea wasi wasi wao juu ya usalama wa maelfu ya raia wanaoishi katika eneo hilo.

Wakati huO huo Ufaransa ilitangaza itafanya mkutano wa kimataifa alhamisi kuzungumzia uthabiti wa wa Mosul baada ya mapambano ya kijeshi.

XS
SM
MD
LG