Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:05

IOM inawasaidia wahamiaji kutoka Libya


Moshi unaotokana na shambulio la anga lililofanywa na ndege za vita za Libya karibu na kituo cha ukaguzi cha upinzani karibu na mji wa mafuta wa Ras Lanouf, mashariki ya Libya, Machi 7, 2011
Moshi unaotokana na shambulio la anga lililofanywa na ndege za vita za Libya karibu na kituo cha ukaguzi cha upinzani karibu na mji wa mafuta wa Ras Lanouf, mashariki ya Libya, Machi 7, 2011

Idadi ya wahamiaji wanaokimbia ghasia huko Libya imeanza kupungua wiki hii ukilinganisha na hali ilivyo kuwa wiki mbili zilizopita, hiyo ni kufuatana na maafisa wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM.

Mamilioni ya wahamiaji kutoka mataifa mbali mbali ya dunia wamekuwa wakikimbilia Misri au Tunisia tangu ghasia za kutaka kumpindua kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Muammar Gadhafi kuanza wiki mbili zilizopita.

Afisa wa habari wa IOM kwenye mpaka wa Libya na Tunisia Jumbe Omari Jumbe anasema, "wiki iliyopita tulikuwa tunawapokea hadi wakimbizi elfu 20 kwa siku lakini hivi sasa kuna takriban wahamiaji elfu tatu hadi elfu nne kwa siku wanaowasili".

Bw Jumbe anasema, mashirika ya kimataifa yanafanaya kazi kwa pamoja kuwahudumia wanaowasili lakini zaidi ni wananchi wa Tunisia wenyewe ambao anasema wamekuwa na ukarimu mkubwa wakiwasaidia kwa hali na mali.

XS
SM
MD
LG