Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 00:35

INTERPOL imemkamata mshukiwa wa uhalifu wa mtandao


Nembo ya INTERPOL
Nembo ya INTERPOL

Maafisa nchini Nigeria wamemkamata kiongozi anayeshukiwa kuhusika na mtandao haramu wa barua pepe ambazo zinawaibia watu mamilioni ya dola.

Idara ya kimataifa ya polisi INTERPOL na tume inayohusika na masuala ya kiuchumi na uhalifu wa fedha ilisema Jumatatu kwamba mwanamme huyo aliyetambuliwa kuwa raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 40 aliyetajwa kwa jina moja la Mike alikamatwa katika operesheni ya pamoja huko Port Harcourt mwezi Juni mwaka 2016.

Taasisi hizo zilisema Mike alimiliki mtandao wa kihalifu wenye watu wasiopungua 40 nchini Nigeria, Afrika kusini na Malaysia ambao walifanya wizi na pia mawasiliano ya biashara haramu ya mzunguko wa fedha nchini China, ulaya na Marekani ambapo walitoa akaunti za benki kwa ajili ya shughuli za fedha taslim.

XS
SM
MD
LG