Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:59

ICC yampata na hatia Thomas Lubanga


Mbabe wa Vita wa Congo Thomas Lubanga, (kati kati) akisubiri uwamuzi wa mahakama ya ICC mjini The Hague, Netherlands, Wednesday, March 14, 2012.
Mbabe wa Vita wa Congo Thomas Lubanga, (kati kati) akisubiri uwamuzi wa mahakama ya ICC mjini The Hague, Netherlands, Wednesday, March 14, 2012.

ICC inatazamiwa kutoa hukumu dhidi ya Bw Lubanga baada ya kumpata na hatia ya uhalifu wa vita katika jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Jaji aliyeongoza kesi Adrian Fulfgord, amesema kwa sauti moja mahakama imeamua kwamba ushahidi, ikiwa ni pamoja na picha za video, na maelezo ya mashahidi, unathibitisha kwamba Bw. Lubanga na washirika wake waliwaandikisha, wakifahamu ni kosa, watoto wa miaka 15 na chini katika kundi lao la vita..

Hakimu amesema, watoto waliandikishwa ili kwenda kupigana katika tawi la kijeshi la kundi lake la Union Congolese Patriots wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya DRC kati ya mwaka 2002 na 2003.

Mbunge wa chama cha Lubanga cha UPC, katika bunge la taifa John Kinazabo ameiambia Sauti ya Amerika kwamba uwamuzi huo haujafurahisha chama kwani wanaamini kuna wengine walohusika na hivyo ni uwamuzi wa kisiasa.

Hiyo ni hukumu ya kwanza kutolewa na mahakama ya ICC tangu kuundwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, na wachambuzi wanasema ni ushindi mdogo lakini, muhimu kwa mahakama hiyo.

Lubanga atabaki jela hadi kesi ya kusikliliza hukumu yake, ambayo inasemekana huwenda akapata kifungo cha maisha. Hata hivyo anaweza kukata rufa dhidi ya hukumu hiyo.

XS
SM
MD
LG