Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:08

ICC yafuta mashitaka dhidi ya Kenyatta


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyefutiwa mashitaka na ICC.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyefutiwa mashitaka na ICC.

Habari zilizofika hivi punde zinasema mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Fatou Bensouda, ametupilia mbali mashitaka dhidi ya Rais wa Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Mapema wiki hii mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ilimpa wiki moja mwendesha mashitaka huyo kuongeza kasi ya uchunguzi ama kuyatupilia mbali mashitaka dhidi ya Rais Kenyatta.

Kesi hiyo iliahirishwa mara kadhaa na mahakama hiyo ya The Hague, na Jumatano ilisema kwamba kuchelewa zaidi kungeweza kuwa kinyume na maslahi ya haki katika mazingira yaliyokuwepo.

Rais Kenyatta alikabiliwa na mashitaka dhidi ya ubinadamu akishutumiwa kupanga ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2007 na mapema 2008. Ghasia hizo zilisababisha vifo vya watu 1,100 huko Kenya na kuwakosesha makazi wengine zaidi ya nusu milioni.

Rais Kenyatta mara kadhaa amesema yeye hana hatia.

XS
SM
MD
LG