Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:42

ICC yamhukumu Bemba miaka 18 gerezani


Kiongozi wa zamani wa waasi la MLC jean Pierre Bemba
Kiongozi wa zamani wa waasi la MLC jean Pierre Bemba

Mahakama ya uhalifu wa kimataifa - ICC - imemhukumu kiongozi wa zamani wa kundi la waasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean Pierre Bemba, jumla ya miaka 18 gerezani baada ya kumkuta na hatia katika makosa matano ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Katika hukumu iliyosoma katika mahakama ya ICC mjini the Hague Jumanne Bemba ambaye aliwahi kuwa makamu rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo atatumikia kiasi cha miaka kumi tu gerezani kwa sababu muda aliokuwa gerezani tangu akamatwe 2008 pia unahesabiwa.

Bemba alihukumiwa miaka 16 kwa mauaji kama uhalifu wa kivita, miaka 16 kwa mauaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu, miaka 18 kwa ubakaji kama uhalifu wa kivita, miaka 18 kwa ubakaji kama dhidi ya ubinadamu na miaka 16 kwa uporaji wa mali kama uhalifu wa kivita.

XS
SM
MD
LG