Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:17

Human Rights watch yawataka viongozi Guinea kuchukua hatua


Wanajeshi wa Guinea wakitoa vifaa vya kupigia kura kwenye ghala iliyoungua
Wanajeshi wa Guinea wakitoa vifaa vya kupigia kura kwenye ghala iliyoungua

Human Rights Watch yawataka viongozi wa Guinea kuchukua hatua dhidi ya waliofanya mauaji ya halaiki na ubakaji

Shirika moja la kimataifa la haki za binadamu limewataka viongozi wa Guinea kuchukua hatua dhidi ya wale waliofanya mauaji ya halaiki na kuwabaka mamia ya waunga mkono upinzani wakati wa maandamano mwaka jana.

Human Rights Watch ilisema Jumatatu kuwa maadhimisho ya mwaka mmoja ya mauaji ya halaiki ya Septemba 28 yanakaribia, lakini hakuna hata kesi moja iliyofunguliwa.

Mtafiti wa juu wa Afrika maghraibi Corinne Dufka alisema kwenye taarifa yake kwamba haki kwa waathirika kwa kile alicokiita vitendo vya kikatili isiachwe ikateleza.

XS
SM
MD
LG