Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:52

Hollande amshinda Sarkozy katika uchaguzi Ufaransa


Mgombea kiti cha rais wa chama cha Socialist Francois Hollande akifuatana na mwenzake Valerie Trierweiler (kushoto) mjini Paris
Mgombea kiti cha rais wa chama cha Socialist Francois Hollande akifuatana na mwenzake Valerie Trierweiler (kushoto) mjini Paris

Francois Hollande akirudisha madarakani chama cha Socialist baada ya kuwa upinzani kwa karibu miaka 25

Rais anaeondoka madarakani Nicolas Sarkozy amewashukuru wafuasi wake na kukiri kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi Jumapili, na kuwa rais wa kwanza kuondolewa madarakani baada ya mhula mmoja.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na vyombo vya habari yanaonesha Bw Hollande akijipatia asili mia 51.9 za kura akimshinda mpinzani wake Bw. Sarkozy aliyepata asili mia 48.1.

Sherehe kubwa zinafanayika katika kila pembe ya Ufaransa usiku wa Jumapili kufuatia ushindi huo ambao wengi walitarajia, na wachambuzi wanassema wapiga kura wa Ufranasa walitake kumondowa Sarkozy kutokana na sera zake za ndani na nje.

Wachambuzi wanasema kutakuwepo na mageuzi makubwa katika sera za ndani na nje za Ufaransa, kwani wakati wa kampeni za uchaguzi Bw. Hollande alieleza upinzani wake mkubwa kutokana na sera za aliyemtangulia.

Akizungumza na Sauti ya amerika mohamed saleh, mchambuzi wa masuala ya kisasa mjini Paris anasema watu wamefurahi sana ushindi wa Hollande aliyeahidi kubuni nafasi zaidi za kazi na kubadili sera ya Ulaya upande wa uchumi.

XS
SM
MD
LG