Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 14:54

Matumaini yaongezeka wakati dunia inaadhimisha siku ya Ukimwi


Wanafunzi wasichana wakiwasha mishumaa mfano wa utepe katika kampeni ya HIV na Ukimwi duniani
Wanafunzi wasichana wakiwasha mishumaa mfano wa utepe katika kampeni ya HIV na Ukimwi duniani

Kwa kipindi cha karibu miongoni mitatu leo Desemba 1, tumekuwa tukisikia habari kuhusu janga la Ukimwi. Wanaharakati kote duniani wanazungumzia virusi vya Ukimwi katika siku hii muhimu. Wanashawishi ufanyike upimaji, kugawa vipeperushi vyenye habari kuhusu HIV, virusi ambavyo vinasababisha Ukimwi, jinsi vinavyosambaa, na jinsi ya kujizuia kuvipata.

Ukimwi umeua takriban watu milioni 35 tangu kuanza kwa ugonjwa huu. Umewaacha mamilioni ya yatima kutokana na janga hili. Kila mwaka watu milioni 2 wanaambukizwa virusi, na Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba zaidi ya watu milioni moja wanafariki kila mwaka kutokana na virusi hivyo.

Bado, mengi yametokea tangu kuadhimishwa kwa mara ya kwanza siku ya Ukimwi duniani mwaka 1988. Nchi ambazo suala hilo liliwahi kuwa mwiko kulizungumzia hivi sasa zinatoa msaada wa upimaji na matibabu. Kina mama wenye HIV wanaweza kujifungua watoto wenye afya njema na kuwalea wao wenyewe. Madawa yanaweza kuvizuia virusi visisambae. Zaidi ya watu milioni 18 wanapatiwa madawa ya kurefusha maisha ambayo yanafuatilia hali yao ya HIV. Hivi sasa wanasayansi wanazungumzia kuhusu chanjo na tiba.

Kiwango kikubwa cha majaribio ya chanjo muhimu yanaendelea nchini Afrika Kusini. Utafiti huu utahusisha zaidi ya wanaume na wanawake 5,400 kati ya umri wa miaka 18 na 35 ambao wanajihusisha katika kufanya mapenzi katika maeneo mbali mbali ya Afrika Kusini, nchi ambayo zaidi ya watu 1,000 kwa siku wanaambukizwa HIV. Majaribio yatadumu kwa kipindi cha miaka minne.

Utafiti unafadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia taasisi ya kitaifa ya afya na magonjwa ya kuambukiza, ambapo Dr. Anthony Fauci ameiongoza kwa kipindi cha miaka 32 iliyopita. Wakati kuna matumaini makubwa kwamba chanjo hii huenda ikasaidia kumaliza tatizo la HIV na Ukimwi, Fauci anaangalia hali halisi. “ hatuna uhakika kama itafanya kazi au la,” amesema. “Chanjo nyingi za majaribio zimeshindikana badala ya kuleta mafanikio –lakini cha msingi ni kuzijaribu na kuona kama zitafanyakazi.”

Mafanikio makubwa yamepatikana tangu siku ya Ukimwi duniani 1988, wakati huo mtu aliyekuwa anaugua Ukimwi alitarajiwa kuishi kwa kipindi cha mwaka mmoja mpaka mwaka mmoja na nusu.

“Leo kutokana na mchanganyikio wa madawa tuna watu ambao, kwa mtu aliye katika umri wa miaka ya 20, na ikiwa ameambukizwa na akifika kupatiwa dawa mchanganyikio, unaweza kubashiri kwamba anaweza kuishi kwa miaka 50 zaidi. Hayo ni maendeleo yasiyo ya kawaida katika kipindi cha mpito kutoka utafiti wa msingi kwa kuingilia katika nyanya yoyote ya madawa,” amesema Fauci.

XS
SM
MD
LG