Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:27

Hillary Clinton kutembelea Afrika


Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nje wa Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, atasafiri wiki ijayo kuelekea nchi tatu barani Afrika, kuzungumzia biashara, maendeleo na masuala ya usalama wa kieneo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema Clinton atatembelea Zambia, Tanzania na Ethiopia, kisha ataelekea Umoja wa falme za kiarabu, ambapo atalenga mgogoro wa Libya.

Clinton amepangiwa kuhudhuria mkutano wa biashara nchini Zambia, utakaofanyika Ijumaa ya Juni 10 na kukutana na Rais wa Zambia, Rupiah Banda. Akiwa nchini Tanzania, wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani inasema Clinton, ataelezea mafanikio ya nchi mbili ikiwa ni pamoja na program kadhaa zilizopo huko.

Clinton anatarajiwa kutembelea Umoja wa Afrika wakati akiwa Ethiopia na kukutana na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Jean Ping. Wakati wa safari yake, Clinton pia atakutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

XS
SM
MD
LG